Friday, September 23, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 55 & 56 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


Mtunzi : EDDAZARIA G.MSULWA


ILIOISHIA....
 “Sali sala yako ya mwisho?”
Dorecy alizungumza huku sura yake ikiwa imejaa jasho jingi, na mikonjo iliyonifanya niamini huu ni mwisho wa maisha yangu mimi Eddy Godwin

ENDELEA....
“Dorecy umechanganyikiwa?”
Nilimuuliza Dorecy anayeonekana kumaanisha kile kitu anacho kizungumza, hakunijibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuendelea kunielekezea bastola yake kwenye sura yangu
“Eddy usimuamini kila unaye muona utaumia sawa?”

Dorecy alizungumza na gafla nikastukia akinipiga na kitako cha bastola kwenye kichwa changu, giza lililo andamana na maruwe ruwe kitanitawala taratibu katika macho changu na kwa mbali nikausikia mlango ukifunguliwa, baada ya muda kidogo sikujua ni kitu gani kinacho endelea  

Nikahisi nikiguswa mgongoni, taratibu nikayafumbua macho yangu na kukutana na viatu vya mwanaume vikiwa vimesimama kando yangu, nikakinyanyua kichwa changu  taratibu huku nikiwa ninamaumivu makali, nikakutana na sura ya mwanaume ambaye amevalia sare za wahudumu wa hoteli hii

“Kaka, habari yako”
Jamaa alinisalimia, huku akinitazama usoni mwangu.Sikumjibu cha kwanza kutazama ni kuangalia sehemu nilipo weka begi langu lenye madini ndani, sikuliona na kujikuta nikikurupuka na kusimama, nikaingia bafuni na kukuta kweupe hakuna mtu

“Kaka vipi?”
“Ku..kunaa dada hiv...i mrefu ume...muona wapi?”
“Yule uliye ingia naye jana usiku?”
“Jana, usiku? Eheee huyo huyo”
Niliungumza huku nikipiga hatua kuelekea kwenye dirisha, nikatamani kuanguka chini na kupoteza fahamu, kwani mwanga mkali wa jua nilio ukuta nje ya dirisha umenichanganya kiasi kwamba nimekosa la kuzungumza

“Yule mbona aliondoka usiku ule ule?”
“Shitii”
“Kwani, hamujuani?”
“Ehee”
“Hamujuani?”
Hata sikujua nimjibu vipi, muhudumu huyu aliye simama mbele yangu, nikajichunguza na kugundua kuna damu zilizo mwagika kwenye shati langu la kiaskari nililo livaa.
“Unamichirizi ya damu puani kaka”

Muhudumu alinionyesha, nikasimama kwenye kioo kilichopo kwenye hichi chumba na kujikuta ni kweli nilitokwa na damu za puani, ambayo kwa sasa imekauka.Muhudumu akanipatia  taulo na nikaanza kujifuta
“Alafu, kuna askari walinionyesha picha yako mida ya asubuhi, na kuniuliza kama wewe upo kwenye hii hoteli nikwaambia kwamba uliondoka jana usiku”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio, huku wasiwasi mwingi ukianza kunitawala

“Waliondoka?’
“Ndio waliondoka, ila sijajua kama watarudi tena au la”
“Asante ndugu yangu”
Nikatizama chini, na sikuona bastola zangu nikatambua ni lazima Dorecy atakuwa ameondoka nazo zote,
“Kaka kwani wewe ni askari kweli?”
Jamaa aliniuliza, nikamtazama kuanzia juu hadi chini, kwani maneno ya Dorecy aliyo niambia nisimuamini mtu yakaanza kunirejea kichwani mwangu
“Kwani vipi?”
“Nimeuliza hivyo kwa nia nzuri tu?”
“Nia gani?”

“Kwa maana picha ya sura yako, sio mara yangu ya kwanza kuiona kwenye mach yangu”
“Ulisha wahi kuiona wapi?”
“Wewe si ndio, Eddy?”
Sikustushwa sana kwa maana ninatambua kwamba ninatafutwa karibia nchi nzima ya Tanzania kwa tukio la kumuu Derick
“Mimi sio Eddy?”
“Sawa”

Nikatoka nje ya chumba, nikatizama kwenye kordo zote na kuona hakuna dalili ya kuwa na mtu, nikaanza kutembea kwa hatua za haraka kuelekea kwenye ngazi za kushuka chini, nikaanza kushuka kwenye ngazi ya kwanza, nikaisikia miguu ya watu wakikimbia na kunilazimu kuchungulia chini, nikaona kundi la askari wapatao sita wakipandisha ngazi kwa haraka huku wanne wakiwa na bastola na nyuma yao wakiwa wameongozana na mzee mwenye kitambi kwa haraka nikatambua ni meneja wa hii hoteli.Nikarudi juu haraka na kukutana na muhudumu niliyekuwa chumbani
“Tupandishe huku juu”

Aliniambia huku akitangulia kupandisha ngazi za kuelekea ghorofa ya juu, tukapandisha ghorofa ya juu na kutokea kwenye moja ya mlango wenye ngazi za chuma zilizo elekea chini.Tukaanza kushuka kwa haraka
“Huku ni nyuma ya holet”
Aliniambia, tukashuka hadi chini, tukakuta kijimlango kidogo, kilichopo kwenye ukuta na tuapita na kutokea kwenye hoteli nyingine niliyokuta kibao kikubwa kilicho andikwa ‘Macarios Hotel’

“Tupite huku”
Tukakatiza kwenye reli, na kushika barabara ya kuelekea magharibi kwetu na kutukea kwenye barabara moja inayopitisha magari mengi
“Hapa kunaitwa kwaminchi”
“Sawa”
Tukaendelea kukatiza mitaa, na kufika kwenye mtaa mmoja ulio na nyumba nyingi zilizo banana sana

“Hapa ni mwamboni”
“Kupo kama mbagala”
“Kwa nini?”
“Nyumba zake jinsi zilivyo”
“Karibu ndani”
Tukaingia kwenye nyumba iliyo chakaa kiasi fulani, akanikaribisha ndani kwake, ambapo kuna kitanda na kistuli kimoja, pamoja na nguo baadhi
“Karibu kaka”
“Asante”

Nikakaa kwenye kiti na yeye akaketi kwenye kitanda chake
“Kwa jina mimi ninaitwa Mbasa, ni mwenyeji wa bara, mkoa wa Shinyanga huko”
“Ahaaaa, kwanza ninashukuru kukufahamu, pili ninashukuru kwa kunisaidia”
“Kusaidiana ni jamba la kawaida, hususani kwa vijana kama sisi ambao tunatakiwa kuwa bega kwa bega katika kuhakikisha tunafikia kwenye malengo yetu”
“Nikuulize kitu Mbasa?”
“Uliza tuu”

Unawezaje kumsaidia mtu usiye mjua?”
“Kaka Eddy, mimi ninakujua na nimekuwa nikifwatilia habari zako kwenye magazeti jinsi unavyo tafutwa na jeshi la polisi kwa mauaji ya bwana Derick”
Nikamtazama jamaa vizuri, nikajitazama na mimi vizuri nikajisemea kimoyo moyo hata akitaka kuanzisha ugomvi, ninamudu tena sana
“Isitoshe, nilivutiwa sana na wewe”

“Kwa nini?”
“Umri wako na matukio yako uliyo yafanya ni tofauti”
“Sawa, ila ninakuomba usimuambie mtu juu ya uwepo wangu hapa kwako”
“Si wezi kwa maana ninahitaji tusaidiane”
“Tusaidiane?”
“Ndio, shida uliyo kuwa nayo wewe kidogo inaendana na yakwangu?”
“Shida gani”

“Nilizaliwa kwenye familia ya maisha bora, baba alikuwa anamiliki migodi ya madini, alikuwa ni tajiri sana.Ila niliaziliwa peke yangu kwa bahati mbaya mama yangu alifariki kwa ajali ya gari, nilikuwa darasa la sita”

“Baba alilazimika kumuona mwanamke mwengine, ambaye alikuwa ni binti mdogo kiasi na alijaliwa uzuri halisi kutoka kwa Mungu, kutokana na kazi nyingi za baba tangu, alitumia muda mwingi sana kuwa mbali na mama mdogo, ikafikia kipindi nikawa na mahusiano na mama mdogo”

“Badi mama mdogo alipata ujauzito wangu na mbaya zaidi niliwahi kubalehe haraka sana, ule ujauzito tuliulea katika mzingira ya kificho na ninacho mshukuru MUNGU, baba alisafiri kikazi kwenye Ujerumani na alikaa mwaka na nusu so ile ishu hakuijua”
“Mwanangu alizidi kukua pasipo baba kujua hilo, hadi anatimiza miaka mitatu, kama unavyo jua dunia haina siri baba yangu akaja kuligundua lile swala la mimi kuzaa na mama mdogo”

“Huwezi kuamini, kuna siku baba alituomba twende naye shambani, hatukuwa na kipingamizi kutokana tulikuwa hatujui kinacho endelea”
“Ngoja kwanza hapo mtoto wenu mulikuwa mumemuweka wapi?”
“Mtoto, tulimpeleka kwa dada yake yule mama mdogo, pesa za matumizi mimi ndio nilikuwa ninazipeleka pasipo baba kuelewa mchezo”

“Sasa tuifika shambani, tukiwa na mama mdogo, pamoja na baba.Tulikuta watu wake ambao mara chache huwa ninawaona ona, huwezi amini nilimkuta mwangu akiwa ametundikwa juu ya mti huku ngozi yake ikiwa imechunwa kama mbuzi aliye chunwa ngozi”

“Baba, yangu alitugeukia hapo hapo na kuanza kumshambulia mama mdogo kwa ngumi na mateke, huwezi ukaamini nilimshuhudia mama mdogo akichemshwa katika pipa lenye mafuta ya kula, huku akiwa hai, cha kumshukuru MUNGU, niliweza kufanikiwa kukimbia ila niligwa risasi za ya paja na kuanzia hapo sikuweza kumuona baba tena kwenye maisha yangu”

“Ila nilikuja kugundua kwamba baba pia alihusika na ajali ya mama”
“Kisa kilikuwa ni nini?”
“Hadi leo sijajua kisa kilikuwa ni nini hadi baba akaamua kumuua mama”
Nilimsikiliza Mbasa vizuri sana, kidogo yeye ana nafuu sana katika simu lizi ya maisha yake ya nyuma

“Baba yako anaitwa nani?”
“Godwin?”
Nikastuka, na kumtazama vizuri
“Mbona unastuka kaka Eddy?”
“Anaitwa Godwin, yupoje poje?”
“Mrefu kiasi, ni maji ya kunde kidogo, anamwili ulio jazia kidogo na pia anakovu kwenye mkono wake wa kulia, mama aliniambia baba alipataga ajali akiwa kijana”

Sifa ambazo Mbasa alinielezea zifanana na sifa za Mzee Godwin ambaye hapo mwanzo niliamini ni baba yangu ila ukweli ni kwamba ni baba yangu mkuwa, ila kitu kinacho nichanganya ni Mzee Godwin ninaye mjua mimi ni Mwanajeshi

“Ana kazi nyingine anayo ifanya ukiachilia na madini?”
“Ndio, nilikuja kushangaa siku nilipo sikia kwamba amepewa cheo cha kuwa mkuu wa jeshi wakati sijui hata jeshi yeye amekwenda lini?”
Nikajikuta nikishusha pumzi nyingi, nikamtazama Mbasa kuanzia juu hadi chini na kujikuta nikitingisha kichwa kwa kumuonea huruma

“Vita iliyupo mbele yetu ni kubwa sana”
“Kivipi?”
“Mbasa kwanza una umri gani?”
“Miaka ishirini”
Nikatabasamu, tabasamu lililo jaa uchungu kwa kumuonea huruma
“Adui yako ndio adui yangu”
Nilimuambia Mbasa na kumfanya abaki amenitumbulia mimacho.....

                        *****SORY MADAM*****(56)

“Kaka Eddy sijakuelewa bado?”
“Kwa sasa sio rahisi sana wewe kunielewa, ila utakuja kunielewa muda ukiwadia”
Sikutaka kumfafanulia kila kitu Mbasa, zaidi ya kuwa makini sana kwa kila jambo ninalo lizungumza, hii ni kutokana na moyo wangu kupoteza uaminifu juu ya kila anaye nisaidia.

Nikakaa nyumbani kwa Mbasa siku mbili mfululizo pasipo kutoka nje, na kila siku Mbasa akawa na kazi ya kunihadisia hali halisi inavyo endelea nje kuhuasiana na polisi wanao nitafuta, siku ya tatu nikaamua kutoka nje mida ya saa tatu usiku, nikiwa nimevalia nguo za mbasa ambazo kidogo kwangu ni ndogo, ila kutokana sikuwa na lakufanya nikaamua kufanya hivyo.Nikavalia kofia iliyo yaficha macho yangu na moja kwa moja nikaelekea kwenye moja ya baa inayo itwa kilimani, lengo langu ni kupata bia japo mbili ili kuiweka akili yangu sawa

Kama kawaida muhudumu mmoja akanisogelea huku akinitazama machoni mwangu, akisubiria nini niagize,
“Niletee, kilimanjaro ya moto”
“Sawa, naomba pesa”
Nikatoa noti ya elfu tano aliyo nipatia Mbasa mida ya jioni alipokuwa akielekea kazini kwake, kuingia katika zamu ya usiku.Muhudumua akaondoka na haikuchukua dakika nyingi akarejea akiwa na chupa bia niliyo muagiza
“Utatumia glasi?”
“Hapana, asante”

Taratibu nikaanza kuporomosha mafumba kadhaa ya bia, huku sehemu niliyo kaa inakigiza kidogo na nisehemu ambayo ninaweza kuwaona wanao ingia na kutoka kwenye hii baa.Baada ya muda kidogo nikawaona wasicha wawili wa kiarabu wakiingia kwenye baa hii, huku mmoja akiwa amevalia baibui na mwengine akiwa amevalia suruali ya jinzi pamoja tisheti iliyo mbana, wakasimama na kuanza kutazama tazama ni sehemu gani ambayo waneweza kupata viti na kwabahati nzuri meza niliyo kaa mimi ina viti viwili, na sehemu nyingine zimajaa watu.Wakapiga hatua za taratibu hadi sehemu niliyo kaa mimi
“Sahamani, tunaweza kuketi hapa?”
“Ndio munaweza”

Wakaa na mimi nikaendelea kunywa bia yangu ambayo, ninaishuhudia ikielekea ukingoni na muda wangu wa kukaa kwenye hii baa utakuwa umekwisha, ukimya ukatawala kati yetu na hakuna ambaye alimsemesha mwenzake, baada ya wao kugizia vinywaji wakawa na kazi ya kuchezea masimu yao makubwa ya kugusa na kidole

“Muhudumu”
Msichana mmoja alimuita muhudumu aliyekuwa anakatiza karibu yetu
“Mletee huyu kaka,kinywaji atakacho kihitaji yeye”
“Ahaa jamani mimi, hii moja inanitosha”
“Hapana, dada mwaya lete kinywaji kama anacho kitaka huyu kaka”
Sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana nao,

“Mimi naitwa Rajiti na mwenzangu anaitwa Sashah”
“Nashukuru kuwafahamu”
“Jamani hatupaswi kukujua jina lako?”
Nikatabasamu kidogo, huku nikiwa ninawatazama kwa macho ya uamakini kila mmoja kwenye sura yake
“Ninaitwa Thoma”
Niliwaongopea kuhofia jina langu la Eddy kuwa ni miongoni mwa majina yanayo tajwa kila siku katika vyomba vya habari
“Kuna kaka umefanana naye”
Sashah alizungumza, huku akiliiknja vizuri mikono ya baibui lake

“Nani?”
“Anaitwa Eddy”
Moyo ukaanza kunienda mbio huku mapigo ya kawaida yakibadilika na kuwa ya kasi sana kiasi kwamba nikaanza kujihisi vibaya
“Ahh….haaa sio mimi?”
Wakanitazama kwa umakini
“Samanani ninaomba niende msalani”

Nikawaaga na kunyanyuka, nikatamani kutoka nje ya baa ila macho yao yote tapo kwangu, nikamuuliza  muhudumu ni wapi kilipo choo, akanielekeza na bahati mbaya kipo ndani ya baa hii na kama kingekuwa ni nje ingekuwa ni nafasi nzuri ya mimi kuwakimbia.Nikaingia chooni na kusimama kwenye moja ya kioo kilichomo humu ndani, nikaivua kofia yangu na kujitazama vuzuri
“Sijabadilika chochote usoni mwangu”

Nilizungumza kwa sauti ya chini, nikajiweka sawa na kuivaa kofia yangu na taratibu nikaanza kuelekea ulipo mlango, nikakishika kitasa cha mlango huku nikiwa ninahema sana, nikashusha pumzi nyingi na kuufungua mlango, nikapiga hatua mbili, gafla nikastukia nikizibwa pua na kitambaa chenye harufu ambayo tangu nizaliwe sikuwahi kuinusa, mtu aliye nikaba kwa nyma sikujua ni nani, na nilipo jaribu kuminyana naye, ndvyo naye alivyozidi kukikandamiza kitambaa puani mwangu na taratibu nikajikuta nguvu zikiniishia na nikapoteza fahamu.

Kwa mbali nikaanza kuona kitu nikiwa kinazunguka juu yangu, nikajaribu kuyakaza macho yangu, ila bado nikashindwa kuyafumbua, nikutokana na uchomvu mwingi ulio ambatana na usingizi mzito, nikajaribu kuinyanyua mikono yangu ila nikaihisi kuwa ni mizito sana, nikakigeuza kichwa changu upande wa kushoto na kukuta jamaa lenye miraba miine likiwa limekaa kwenye kiti, huku sura yake ikiwa na mindevu mingi sana.Hapa ndipo nilipo anza kugundua kwamba nimelala chali juu ya kindanda, sikuona kitu chochote kilicho ufunga mkono wangu, na sikuelewa ni kwanini nimekuwa mchovu kwenye mikono kiasi hichi.

Nikaendelea kuvuta kumbukumbu ya nimefika vipi katika eneo hili, ila ubongo haukusoma kitu chochote zaidi ya kukumbuka kwamba nilikuwa nipo baa.Baada ya masaa kadhaa nguvu za mwili wangu zikaanza kurejea taratibu, nikapata nguvu hata ya kuyafumbua macho yangu hapo ndipo nikagundua kitu kinacho zunguka juu yangu ni feni
“Nipo wapi?”
Nilimuuliza jamaa, hakunijibu chochote zaidi ya kunitazamaa kwa macho makali, hukua akiendelea kuzichezea ndevu zake nyingi nyingi

“Nipo wapi?”
“Wee koma”
Jamaa alizungumza huku akininyooshea kidole, akionekana kukasirishwa na swali langu nililo tumia sauti ya ukali kumuuliza.Akasimama na kuitoa simu yake ya mfukoni
“Mtu wenu ameamka”

Sikujua anazungumza na nani, mapigo ya moyo yakaanza upya kudunda huku yakiandamana na wasiwasi  mwingi, wazo la kwanza kunijia kichwani nikajua tarari nimeingia kwenye mikono ya Mzee Godwin, nikajaribu kusimama ila jamaa kwa haraka akaniwahi kunisukuma kitandani

“Ukilete ujinga jombaa nitakupoteza duniani?”
Nikazidi kuchanganyikiwa, baada ya muda wakaingia Rajiti na Sashah, wote wawili wamevalia suruali nyeusi na tisheti nyeusi, huku miguni wakiwa wamevaa, buti nyeusi
“Habari yako, Eddy?”

Rajiti alinisalimia, hapo ndipo nikadata kabisa na kutambua kwamba hawa si watu wazuri kwangu, kutokana niliwatambulisha kwa jina la Thomas, inakuwaje wananiita mimi Eddy

“Kamletee chakula”
Jamaa likatoka na kutuacha ndani ya chumba
“Eddy ninaimani utajiuliza imekuwaje hadi upo hapa” Sashah alizungumza
“Ndio”
Rajit akatoa picha mfukoni na kunirushia mimi kitandani nilipo lala, picha aliyo nirushia ina sura yangu na mama yangu zikiwa zimeambatanishwa kwa pamoja na kuitoa picha moja

“Usishangae sana, na kujiuliza ni wapi tumeitoa picha yako, kwa ufupi sisi tulikufwatilia kwa siku nyingi hadi jana tulipo fanikiwa kukupata” Rajit alizungumza
“Munataka nini kutoka kwangu?”
“Kikubwa tunacho kihitaji sisi ni wewe kukusaidia”
“Kunisaidia kivipi?”
“Utaelewa”
“Sisi ni wanajeshi wa kikundi cha Al-khaida, na kazi yetu kubwa ni kutafuta vijana wenye matukio makubwa kama yako, pia isitoshe tunahitaji kukupa msaada wa kumpata mama yako”

Baunsa akaingia huku akiwa amebeba sahani kubwa yenye vitu mbali mbali vya kufungua kinywa, akaviweka kwenye meza na kutoka nje
“Tunahitaji tukupeleke Iraq, yalipo makazi yetu kisha ukirudi Tanzania tukusaidia kwenye kazi moja tu”
Rajit alizungumza
“Kazi gani, unajua hadi sasa hivi sijawaelewa?”
“Eddy fungua akili yako, Tanzania nzima unatafutwa wewe, 
Je ukikamatwa ni wapi utapelekwa?”
“Gerezani” Nilimjibu Rajit
“Je upo tayari kuishi, gerezani?”
Swali la Rajiti likanifanya nikae kimya pasipo kumjibu chochote
“Hapa kwani nilipo ni wapi?”
“Hapa ni Mombasa, nchini Kenya.Jana tulisafiri usiku kucha hadi hapa”
“Kwa nini muniteke?”
“Ilitulazimu”

Rajiti na Sashah wakendelea kunishawishi hadi nikakubali kwenda nao Iraq kwani nikiangalia kwa jinsi maisha yangu yalivyo ya kuruka ruka kama ndege nikaona ipo siku nitanaswa kwenye jumba bovu.Akaja daktari mwenye asili ya kiarabu, waliye niambia anahusika na kazi ya kuchonhesha sura bandia, dakatari akanifanyia vipimo vya haraka na kazi ya kuchongesha sura nyingine itakayo kaa sawa kwenye uso wangu ikaanza mara moja.
Ndani ya masaa sita tarari daktari akawa ameikamilisha kazi aliyo agizwa na Sashah.Kazi ya kupandikizwa sura bandia ikaanza mara moja, huku daktari akiifanya kwa umakini wa hali ya juu, haikuchukua muda mwingi sana kuvishwa sura bandia, nikaa lisaa moja kwenye kifaa ambacho daktari aliniambia kinaghusika na swala zima la kuikausha sura yangu mpya.

Baada ya zoezi zima la kubadilishwa sura kuisha, Rajiti akanipa kioo niitazame sura yangu niliyo pandikizwa juu ya sura yangu halisi, sikuyaamini macho yangu kwani nimebadilika kupita maelezo hata mimi mwenyewe nikajisau

“Ebwaane eheee ni mimi kweli au naota?”
“Ni wewe, mbona hapo umetokelezea”
“Etii eheee?”
“Ndio”
“Hahaaaa”
“Sashah yupo wapi?”
“Amekwenda Mjini mara moja”
Sashah akarejea akiwa na furaha sana usoni mwake,

“Vipi kitu kimetiki nini?” Rajiti aluliza
“Ndio, chezea mimi wewe”
Rajiti akamkbidhi Sashah hati tatu za kusafiria, na akaanza kuzisoma taratibu
“Kweli wewe kiboko, kitu feki kama orijino”
“Ahaa, kila kitu kinawezekana duniani”
“Ila kipo kisicho wezekana” nilichangia mada
“Kama?”
“Kutengeneza pumzi ya mtu”
“Kweli”

“Mpe Eddy aone passport yake jinsi nilivyo itengeneza”
Sashah akanikabidhi hati yangu ya kusafiria iliyo na sura yangu mpya, huku jina langu likiwa ni Suleima Bin Yahaya
“Mbona jina ni hili?”
“Nisingeweza kuweka jina lako kutokana na wewe kuwa muhalifu, hapa mwenyewe nimetoka Jomo Kenyeata Airport na kuzikuta picha za sura yako zikiwa zemebandikwa kwamba unatafutwa”

“Mmmm”
“Unaguna? Tutakwenda na utaziona”
“Sawa bwana”
“Eheee umekata tiketi ya ndege ya saa ngapi?” Rajit aliuliza
“Saa sita uskuku”
“Ipo powa”
Tukaendelea kupiga stori za hapa na pele na nikawasimulia mkasa mzima wa nyuma uliopita kwenye maisha yangu, hadi ninamaliza wote machozi yakawa yanawamwagika
“Eddy pole sana”
“Asante”

Sashah na Rajiti wakabadilisha mavazi na kuvalia sketi ndefu nzuri na kuwafanya wapendeze sana, huku na mimi nikivalia suti kali waliyo nipa cha kushukuru Mungu imenikaa vizuri mwilini mwangu na kunifanya nionekane kama muheshimiwa wa kitengo fulani cha serikali.Tukaanza safari kwa kutumia usafiri wa gari yao ndogo, inayokwenda kwa kasi sana, kutokana ni usiku hapakuwa na magari mengi sana barabarani,Tukafika katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata, sote tukashuku na zimesalia dakika ishirini kabla ya ndege tunayo ondoka nayo kupaa angani.
Moja kwa moja tuakelekea sehemui ya ukaguzi wa hati za kusafiria, Rajiti akawa wa kwanza kukaguliwa hati yake pamoja na mwili wake kwa kutumia kifaa cha ulinzi, akapita na kupewa hati yake iliyo tiwa muhuri na muhudumu wa kike anaye ifanya kazi hiyo huku akionekana kuwa makini sana, akafatia Sashah akakaguliwa kama alivyo fanyiwa Rajit na akafanikiwa kupia.

Nikamkabidhi msichana hati yangu ya kusafiria cha kwanza akanitazama machoni, kisha hati yangu ya kusafiria akaiweka kwenye mashine inayotoa ripoti kwenye kioo kikubwa cha ‘computer’.Askari anaye kagua akaanza kazi yake ya kukipitisha kifaa chake kuanzia miguuni, msichana akanitazama kwa macho makali kisha akatazama tena kwenye kioo cha kumputer yake, nikatazama pembeni na kuwaona askari wawili walio shika mbwa wakubwa weusi wakianza kunisogelea, huku wakiwa na bubduki zao mikononi, kifaa cha ukaguzi kikaanza kutoa mlio wa kelele huku kikiwaka taa nyekundu kilipo fika maeneo ya shingoni..

 ITAENDELEA...
 Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!