Friday, October 28, 2016

Hukumu ya kunyongwa hadi kufa iliyotolewa kwa wauaji wa Albino Bukoba

Mahakama kuu Kanda ya Bukoba imewahukumu kunyongwa hadi kufa Pankras Minago na Lameck Bazil baada ya kupatikana na hatia ya kumshambulia na kumuua kwa kumchoma na vitu vyenye ncha kali na kunyofoa baadhi ya viungo vyake mlemavu wa ngozi, Magdalena Andrew aliyeuawa September 21 2008.

Hukumu hiyo iliyotolewa na jaji Firmin Matogolo ni ya kwanza katika mahakama kuu kanda  ya Bukoba dhidi ya washtakiwa wa makosa ya mauaji ya watu wenye ualbino. 

Unaweza kuangalia video hii hapa chini kwa hisani ya Azam TV.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!