Sunday, October 2, 2016

Mechi za Simba na Yanga zapigwa marufuku kufanyikia uwanja wa Taifa

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ametembelea Uwanja taifa Jumapili hii na kuzipiga marufuku mechi zote za Yanga na Simba kufanyikia uwanjani hapo kutokana na uharibifu wa mageti na viti uliojitokeza siku ya jana katika mechi hiyo ya watani hao wa jadi.Mashabiki wa Simba wakitawanywa kwa mabomu ya machozi hapo jana baada ya kufanya uharibufu wa viti
 
Pia Nape amezuia mapato ya timu hizo ya mchezo wa jana kutokana na uharibifu huo.
“Simba na Yanga hawatoutumia tena uwanja huu mpaka pale Serikali itakapoona kuwa mazingira yanaruhusu,” alisema Nape. alisema Nape.

Amri hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya mashabiki wa klabu ya Simba, kung’oa viti vilivyopo kwenye majukwaa ya uwanja huo kwa kile walichokidai kupinga uamuzi wa Refa, Martin Saanya aliyechezesha mechi hiyo. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!