Thursday, October 13, 2016

Raymond azungumzia mpango wa kuanzisha label yake ‘WCB haimzuii mtu’


Msanii wa muziki kutoka WCB, Raymond ‘Rayvanny’ amefunguka kwa kusema kuwa msanii akiwa chini ya label ya WCB hakatazwi kuanzisha label yake na kusimamia wasanii.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Natafuta Kiki’, Jumatano hii amekiambia kipindi cha Uhurufleva kinachoruka Uhuru FM kuwa kwa hatua aliyofikia hashindwi kuanzisha label ya kumsimamia wasanii.

“Kila kitu kwenye maisha kinatokea kwa sababu, na katika maisha lazima uwe na mipango. Unajua alichokifanya Diamond pamoja na team yake, Mkubwa Fella, Babu Tale pamoja na Sallam ni kitu kikubwa sana,” alisema Rayvanny “Lakini kuwa na wasanii wangu pamoja na label hayo mambo yanawezekana, WCB haimzuii mtu,”

Aliongeza, “Naweza nikawa na WCB na nikawa na label yangu lakini lazima niangalie. Tunamuona Kanye West yupo kwa Jay Z lakini ana wasanii wake na vyote amefanya kutokana na nafasi yake. Kwa hapa nilipo sishindwi kumsimamia msanii, kumlipia video, kumlipia audio. Pia sishindwi kumfanyia msanii promotion, lakini nikisema nimchukue msanii nimsimamie sasa hivi nitafika sehemu tu nitanasa, kwa sababu kumsimamia msanii sio tu kumlipia video na audio, kuna mambo mengi,”

Pia muimbaji huyo amesema wimbo ‘Salome’ aliyoshirikishwa na Diamond ni wimbo ambao umemtangaza zaidi kuliko nyimbo zake za nyuma.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!