Sunday, October 2, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 61 & 62 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa


Ilioishia...
Khalid akachomoa bastola yake na kumnyooshea mtu huyo, ila kabla hajafyatua akamkabidhi dorecy bastola na kumuomba amuue mtu huyo, dorecy bila ya huruma akafyatua risasi zilizo tua juu ya kichwa cha mtu huyo na kumsababishia kifo, nikashusha pumzi nyingi, kwani dorecy amekuwa katili kiasi cha kuua mtu pasipo kuwa na huruma ya aina yoyote, nikiwa nifikiria cha kufanya nikastukia kitu kigumu kikinigusa kichwani mwangu, na kusikia sauti ya mwanaume ikiniamrisha nilale kama nilivyo na nisifanye kitu chochote la sivyo atauchangua ubongo wangu, taa kubwa lenye mwanga mkali likageukia sehemu ya sisi tulipo, juu ya ukuta na kuwafanya khalid, dorecy na watu wake kutuona.Na khalid akaagiza mtu huyo kunishusha kwenye ukuta.

Endelea....
....Nikashusha pumzi taratibu, jamaa akanigusa tena na ndunduki yake kwenye kichwa changu na kuniamrisha kushuka kwenye ukuta, kwa haraka sana nikajigeuza na kuichota miguu yote ya mtu huyo na kumfanya aangukie ndani kama mzigo wa kuni, nikajirusha na kuangukia nje ya sehemu ambayo nimetokea, cha kumsukuru mungu sijaumia sehemu yoyote ya mwili wangu ambayo itanizuia mimi kukimbia.
Nikanyanyuka haraka na kuhakikisha bastola yangu ipo sehemu nilipo iweka nikaikuta ipo.Kelele za ving’ora vya hatari vikanifanya nianze kukimbia kwa kasi zangu zote na kutokomea msituni, kelele za mbwa wengi, nikaanza kuzisikia nyuma yangu, na kadri ninavyo kimbia ndivyo jinsi zilivyo zidi kuja nyuma yangu kwa kasi kubwa.Milio ya bunduki ikazidi kunipa changamoto ya kukimbia kwani watu wa khalid wapo nyuma yangu, nikajibanza kwenye moja ya mti baada ya kuona risasi zinazidi kuwa nyingi nyuma yangu.Kundi kubwa la walinzi wa khalid wakazidi kunifwatwa kwa nyuma.

“mungu bariki”
Nimaneo niliyo yasema kimya kimya moyoni mwangu, kisha nikaanza kujibu mapigo ya risasi niazo rushiwa kwa fujo, nikaendelea kuwafatulia watu wa khalid na kuwaangamiza kila ambaye nilimfyatulia risasi.

Nikastukia kuona mwanga mkali wa ukinimulika kutoka juu, nikatazama na kukuta ni helcoptar, nikaanza kusikia sauti kutoka kwenye kipata sauti ikiniomba nijisalimishe la sivyo nitauawa kwani sehemu nzima ya msitu imezingirwa, nikaitoa magazine ya bastola yangu na kukuta imebakiwa na risasi moja tu, na nyuma yangu kundi la watu wasio pungua ishirini, wananifwata kwa kuyata, huku wengine wakiwa awanatokea mbele yangu.
Mwanga wa helcoptar ukaendelea kunimulika kiasi cha kuninyongonyeza kabisa katika kupata matumaini ya kujiokoa.Sikuwa na jinsi zaidi ya kupiga magoti chini, huku miono yangu nikiwa nimeiinyoosha juu.Jamaa wakanizingira na wawili wakanisogelea nakuanza kunipapasa na kunitoa kila kitu nilicho kuwa nacho mfukoni mwangu kisha wakaninyanyua na kunifunga waya mgumu kwenye mikono yangu na safari ya kuelekea ilipo ngome ya khalid ikaanza.

Ilituchukua mwendo wa dakika zisizo pungua kumi hadi kufika ilipo ngome ya khalid, nikamuona dorecy na mume wake wakiwa wamesimama kwenye moja ya ngorofa kubwa lililopo ndani ya ngome, macho yao yote yakiwa kwangu
“ohooo karibu bwana eddy”

Muyo ulinistuka sana baada ya kumsikia khalid akizungumza kiswahili kizuri tu, kwa haraka nikayafikira maneno ya kejeli niliyokuwa ninazungumza na mke wake, nikiamini kwamba khalid aelewi kitu ambacho ninakizungumza na mke wake.
“naona umekuja kunitembelea, za masiku bwana eddy?”
Sikumjibu khalid zaidi ya kumtazama kwa macho makali katika sehemu ambayo amesimama, pamoja na mke wake
“mpandisheni huku juu”

Aliwaamuru watu wake na wakaniingiza kwenye moja ya lango kubwa, tukaanza kupandisha ngazi kuelekea ghrorofani, wasiwasi wangu mkubwa ni juu ya mke wangu phidaya, sijui akiamka asubuhi na kunikuta sipo ndani chumbani, ataamua kufanya maamuzi gani.
“karibu eddy, ninafurahi sana kukuona hapa, kwa kipindi hichi kingine.Vipi ulikuwa umekosea njia ya kuja hapa?”

Macho yangu yakagongana na dorecy aliye valia dera refu, kutokana na ujauzito wake kuwa ni mkubwa.Khalid akazitazama ishara za macho kati yangu na dorecy kisha akatabasamu.
“naamini, mke wangu atakuwa na furaha sana kukuona hapa mwanadarasa wake, na munavyo onekana mulikuwa munasoma sana eheee”

“hee baby, hembu acha maneno yako, mimi huyo eddy hatukuwa na ushirikiano kwenye masomo”
Dorecy alizungumza kwa sauti nyororo iliyo mbembeleza mumewe, na taratibu akamsogelea mumewe na kuanza kuzichezea nywele za kifua cha mume wake
“ohh mke wangu, sawa ila vipi, sijaielewa maana ya rafiki yako kuwa hapa?”

“hata mimi sijui”
“eddy, ni kwanini upo hapa?”
“dorecy nipe mali yangu niondoke”
Nlizungumza kwa sauti nzito, na kumfanya khalid kumgeukia mke wake
“anakudai?’
“ahaaa hapana ila sijui kachanganyikiwa huyo”
“eddy, unamdai nini mke wangu?”

Kwa haraka dorecy akanikonyeza, pasipo mume wake kumuona, nakuniomba nisizungumze kitu chochote mbele ya mume wake.Nikatabasamua na kumtazama khalid
“hapana, ile siku nilipo kutana na nyinyi kule dukani, dorecy aliniambia kwamba siku moja nije kuwatembelea atanipa mali ya kutosha”

“ohhh, mke wangu ni mali gani unataka kumpa eddy?”
“ni mtaji wa kufungua biashara, siku ile baby si nilikuwambia kwamba kuna bishara ya hoteli nataka kwenda kuifungua tanzania, so nikaona mtu wa kumuweka awe eddy kama msimamizi”
“ahahaaaa hapo nimewaelewa, kwani mulianza kunitisha.Mfungueni”

Khalid aliwaamrisha watu wake wanifungue mikono yangu na wakatii kama bosi wao alivyo agiza, wakanifungua mikono yangu na akawaomba waondoke, khalid akanikaribisha sebleni kwake, na tukaanza kuzungumza mambo mbalimbali ya maisha, jambo ambalo lilianza kunishangaza kwani khalid niliye adisiwa na muendesha taksi sio huyu ninaye zungumza naye mbele yangu.
“bwana eddy, kunabinti atakuja hapa kukuonyesha chumba cha kulala, mimi ngoja nikapumzike na mke wangu, si unamuona jinsi hali yake ilivyo?”
“hakuna shida shemeji”

Khalid akanyanyuka na dorecy na kupandisha ngazi kwenda juu kabisa, macho yangu yakawa na kazi ya kuwachunguza walinzi walio simama kwenye kila kona ya jumba huili kuanzia ndani hadi nje.Akaja dada mmoja aliye valia chupi aina ya bikini na sidiria

“nifwate”
Alizungumza kwa kingereza, pasipo kuuliza ni wapi ninapo elekea nikanyunyuka na kuanza kumfwata kuelekea sehemu anapo kwenda, tukapita kwenye moja ya kordo ndefu, nyenye wingi wa vyumba kila kona, akafungungua mlango mmojana na sote tukaingia.
“unapenda nini, whyne, shampen, wicky au juis”

Aliniorodheshea idadi ya vinywaji ambavyo sivitumii kwa wakati huu ambao nipo kwenye ngome ambayo hadi sasa hivi sijajua usalama wangu upo kaika upande gani,kati ya kutoka salama au kutokamu ndani ya ngome hii.
“sihitaji chochote, asante sana”
“una hitaji huduma ya mwili wangu”
“hapana ninashukuru”

Baada ya msichana kumjibu hivyo akajizoa zoa na kutoka ndani ya chumba changu na kuniacha nikiwa ninamawazo sana, nikazima taa za chumba kizima na kuwa giza totoro, nikaanza kuchunguza kuta moja baada ya nyingine, kutazama kama kuta kuwa na kamera zilizo fichwa kwenye kuta za chumba hichi, ambazo mara nyingi baadhi huwa zinachimbiwa ukutani, na zinatoa mwanga mwekundu kila unapo ziona kukiwa na giza.
Nikamaliza kukizunguka chumba kizima na sikuona kitu cha aina yoyote, nikaipanga mito mitatu kitandani kama mtu aliye lala na kuifunika kwa shuka.Nikalisogelea dirisha taratibu na kulifungua, ukimya mwingi umetawala nje, kitu kikubwa ninacho kiona ni walinzi wakikatiza katiza kila kona ya ngome hii.

Kitu ambacho kinanifanya nishindwe kushuka kwenye chumba hichi ni kutokana, chumba kipo ghorofani na chini ni mbali sana, mwanga wa jitaa kubwa ukakatiza kwenye dirisha nililo simama na kwa haraka nikajibanza kwenye ukuta ili upite vizuri na walinzi wasione.Ukarudi tena ulipo tokea, kabla sijanyanyuka mlango wa chumbani kwangu ukafunguliwa taratibu na nikamuona  dorecy akiingia huku akiwa amevalia kagauni kakulalia
“eddy”

Aliniita kwa sauti ya kunong’oneza, huku akielekea kitandani ambapp nimepanga mito vizuri kama mtu aliye lala.Akasimama pembeni ya kitanda changu, niaamini hakuniona kwenye sehemu niliyo simama, akakitazama vizuri mwili wa mito nilio ulaza kisha akakipandisha kigauni chake juu, na kuchomoa kisu kikali alicho kuwa amekificha kwa kukifunga kwenye paja lake kwa mpira kisha kwa haraka akakishusha na kutua kwenye mito jambo lililo nistua sana kuona dorecy akizidi kuwa katili juu yangu....


                             *****sory madam*****(62)


.....Dorecy akastuka baada ya kuona kisu kikinyanyuka na mto, ikamlazimu kufunua shuka kwa haraka kwa ajili ya kutazama kama kitandani kwangu kuna mtu, akajikuta akistuka zaidi baada ya kukuta ni mito ndio imejipanga, kwa haraka nikamrukia na kumsukimiza kitandani na kisu chake kikaangukia pembeni, nikakiwahi kukiokota kisu chake, kisha nikamuwahi kulikamata koo lake na kuliminya kwa nguvu  zangu zote huku kisu nikiwa nimekinyanyua juu kwa mkono wangu wa kulia

“unataka kuniua ehee”
Nilizungumza kwa hasira huku nikiendelea kuliminya koo lake na kumfanya atoa mlio wa kukoroma akishiria kukata roho
“e…ddy naa….”

“hakuna cha kuomba, malaya mkubwa wewe, leo ndio utaijua jina langu la utotoni nilikuwa ninaitwa nani”
Niliendelea kukaba dorecy koo lake, hadi akaanza kulegea, nikamuachia na kwaharaka nikashuka kitandani na kuivuta miguu yake na akaangukia mgongo kwenye sakafu, nikamnyanyua juu na kumpiga kabali kwa nyuma huku kisu changu nikikiweka kwenye tumbo lake.
“eddy mpenzi wangu naomba unisamehe nilikuwa ninakutania tuu”

Dorecy alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.Sikutaka kuzisikiliza porojo zake kwa maana hakuna utani wa kuuana
“ongoza njia”
“eheee”
“ongoza kwenda nje”

Nilizungumza huku nikikikandamiza kidogo kisu kwenye tumbo lake lenye mtoto ndani na kumfanya aanze kutambea huku mwili mzima ukimtetemeka, akafungua mlango, na kukutana na walinzi wawili wenye bunduki wakiwa wamesimama kwenye mlango wa chumba changu, hapo ndipo nikagundua kwamba  nilikuwa ninalindwa nje nisitoke.Wakanielekezea bunduki zao, ila mimi nikazidi kumkaba kabali dorecy huku kisu nikikikandamiza kwenye tumbo lake.
“waambie washushe bunduki zao la sivyo nakufanyia oparesheni bila ganzi”

Dorecy akawaamuru watu wake waweze kufanya kama nilivyoa mauambia, wakatii kwa haraka, tukaanzaa kutembea kwenye kordo ndefu ya vyumba, huku walinzi wake wakitufwata kwa nyuma, sikuwa na woga wa aina yoyote kutokana bosi wao yupo chini ya mamlaka yangu.Tukafika sebleni na kukutana na walinzi wapata kumi wakiwa na bunduki zao wakitusubiria sisi kutokea kwenye seble hii.

“eddy, sasa nimeijua rang yako”
Sauti ya khalid ikanistua, nikamuona akitokea kwenye moja ya chumba huku akiwa amevalia nguo za kulalia na mkononi mwaka akiwa ameshika bastola
“waamrishe watu wako kutupisha la sivyo ninamuua mke wako”

Nilizungumza kwa sauti kubwa, huku nikiendela kukikandamiza kisu kwenye tumbo la dorecy ambaye muda wote machozi yanamwagika, kwa ishara khalid akawaamrisha watu wake kutupisha, tukapita katikati yao huku muda wote nikiwa makini sana, nikiwatazama watu wa khalid

“ila eddy unacheza makida makida kwenye nyaza za umeme”
Khalid alizungumza kwa kujiamini sana, sikujali maneno ya khalid zaidi ya kumuamrisha dorecy kutembea kuelekea nje.Tukafunguliwa mlango na walinzi wake baada ya dorecy kuwaamrisha waweze kufanyan hivyo.
“magari yenu yapo wapi?”

Nilimuuliza dorecy kwa sauti ya ukali, taa kubwa lililopo katika jumba hili likawa na kazi ya kutumulika kila sehemu ambayo tunakwenda, macho yangu yote yakawa na kazi ya kutazama kila sehemu ya jengo hili kuangalia walinzi walio jipanga huku wote bunduki zao zikiwa kwetu, dorecy akanionyesha moja yan jengo ambalo aliniambia kwamba ndipo yalipo magari, kwa hatua za umakini tukatembea hadi lilipo jengo hilo na kuingia ndani, ambapo nikakuta magari mengi ya kifahari takiwa yamepangwa kwa mpangilio mzuri.
Macho yangu yakatua kwenye gari aina ya bmw inayo endana na gari ya sheila aliyo pewa na wamarekani alio cheza nao filamu ya ngono.Nikaisogela huku nikiwa ninaendelea kumshika dorecy shingo yake, nikajaribu kufungua mlango wa gari na ukafunguka, kwa bahati nzuri nikakuta funguo ikiwa kwenye siti ya dereva.

“eddy si umesha fika sehemu uliyokuwa unahitaji, niachie sasa”
“bado unakazi na mimi”
“kazi gani jamani eddy?”
“utaijua mbele ya safari”

Nikamshukumiza dorecy kwenye siti ya pembeni na mimi nikaingia, nikaiwasha gari na ikawaka pasipo tabu yoyote, cha kushukuru mungu mafuta ya gari yamejaa vizuri kwenye tanki lake, nikashusha pumzi nyingi huku nikijifunga mkanda wa gari
“eddy khalid atakuua”

Dorecy alizungumza kwa sauti ya chini huku, machozi yakiendelea kumwagika, sikutaka kumsikiliza sana dorecy, nikairuduisha nyuma gari na kuiweka sawa kuelekea kwenye mlango wa kutokea kwenye jumba hili ambao ni wambao.
“funga mkanda”

Nilimuamrisha dorecy na akatii, nikaknyaga mafuta pamoja na breki na kuifanya matairi ya nyuma ya gari kuserereka kwa nguvu, nikaachia breki na kuifanya gari kuanza kwenda kwa mwendo wa kasi, nikaubamiza mlango na gari ikapita kwenye mlango bila ya shida.Taa kali zikapiga kwenye kioo cha gari langu na kunifanya nisione mbele vizuri, nikajikuta nikikanyaga breki kwa haraka, huku macho yangu yakikitazama ‘kifaru’ kikubwa kilichopo mbele yatu.Nikatazama pembeni na kuona kuna bustani ya maua ambayo gari linaweza kupita pasipo shida yoyote.Nikatazam kifaru hichi ambacho mara nyingi hutumika jeshini katika vita.Mwanga wa helcoptar ukaendelea kumulia kwenye gari letu,
“shiti”

Nikakanyaga mafuta kwa haraka, kugeuza gari kwa kasi na kuuelekezea kwenye bustani ya maua, risasi nyingi za walinzi wa khalid zikaanza kupiga kwenye gari yetu cha kushukuru mungu hakuna risasi hata moja ambayo inaingia kwenye gari, nikaendelea kuipitisha gari kwenye bustania ya maua hadi nikafika kwenye barabara kubwa iliyopo ndani ya hili jengo la khalid
“njia hapa ya kutokea ni ipi?”
“wewe nyoosha tuu mbele”

Dorecy akanipa ushirikiano mzuri paiso kupinga, nikazidi kunyoosha kwenye barabara aliyo seme dorecy, huku mfululizo wa risasi ukizidi kuniandama kwa nyuma, mwanga wa helcoptar ukazidi kutumulika

“kunja kushoto”
Dorecy alizungumza na mimi nikafanya kama alivyo seme, kazi yangu kubwa ikawa ni kubadilisha gia kwenye gari na kuongeza mwendo kasi wa gari
“kulia”

Nikakunja kulia kwenye kibarabara kidogo ambacho kwa mbele yake kuna geti dogo lililo wazi, nikazidi kuongeza mwendo kasi wa gari na kutoka kwenye ngome ya khalid.Tukatokea kwenye barabara iliyopo kwenye kilima, huku pembeni ya barabra kukiwa kuna maporomoka marefu mithili ya barabara ya mlima kitonga uliopo mkoni iringa nchini tanzania.
“unaijua hii barabara?”
“ndio wewe twende”

Umakini wote nikazidi kuuweka kwenye barabara, kwani ina kona nyingi, na endapo nitafanya ujinga wa aina yoyote gari itabingiria kwenye maporomoko na ndio utakuwa mwisho wa maisha yangu na dorecy.Helcoptar ya watu wa khalid ikazidi kutufwata kila sehemu ambayo tunaelekea, kutokana na uzoefu wangu wa kuendesha gari kwenye barabara zenye makona mengi, haikuwa nguma kwangu kuhimili kona za hapo kwa hapo ambazo ni nyingi sana.
“ukimaliza kona mbili hapo mbele kuna mporomoko mrefu kuwa makini”

Dorecy alizungumza, ushirikiano wake sikuuamini sana kutokana na yote aliyo nifanyia, nikazidi kuongeza mwendo kasi wa gari huku miguu yangu, ikiwa na kazi ya kucheza na breki.Tukafika kwenye kiporomoko ambacho dorecy anazungumza kwa mbali kidogo nikaona taa za gari kwa haraka haraka zinapata kumi zikiwa zimeziba njia, kwa jicho langu la kushoto nikamuona dorecy akitabasamu hapo ndipo nikagundua amaniuza, kwa kutumia kisukusuku changu cha mkono wa kushoto, nikambamiza nacho dorecy pembeni ya shingo yake na kumfanya atulie kimya na kupoteza fahamu.Nikafunga breki za gari langu, umbali kidogo kutoka zilipo gari za watu wa khalid, nikatazama kushoto kwangu ambapo kuna maporomoko marefu, hapakuwa na nyia ya aina yoyote.Kulia kwangu kuna ukuta mkubwa wa mlima, helcoptar ikasimama na kuzidi kutumulika,

“nitafanyaje?”
Nilijikuta nikijiuliza swali mwenye pasipo kupata jibu, kwa kutumia kioo cha pembeni nikaona gari nyingi zikija kwa kasi nyuma yangu, huku zikaanza kushuka kiporomoko ambacho ndipo nilipo.

“bwana eddy jisalimishe, wewe mwenyewe”
Niliisikia sauti ya khalid ikitokea kwenye kipaza sauti juu ya helcoptar yake,
“siwezi kufa kijinga”
Nilizungumza mwenyewe huku nikiitazama helcoptar ambayo inaendelea kumulika mwanga kwenye gari yetu
“moja jisalimishe”

Khalid alianza kuhesabu, nikatimaza pembeni upande wa kushoto nikaona tobo kubwa kwenye gemo kubwa la mlima, gari za mbele yangu zikaanza kupandisha kilima huku za nyuma zikishuka kwa kasi, nikakanyaga mafuta, pamoja na breki zote kwa pamoja na kuyafanya matairi ya nyuma yakiserereka kwa nguvu gari za nyuma zilazidi kunisogelea katika sehemu ambayo nimesimama, kwa kasi nikakunja kulia na kuifanya gari yangu kuelekea kwenye tobo lilipo kwenye gemo la mlima, sikuamini kama gari yangu inaweza kuingia ndani ya tobo hili, sikumini macho yangu baada ya kukuta barabara iliyo chongwa ndani ya shimo hili, ambayo ipo ndani ya mlima
“waoooo”

Nilijikuta nikipiga kelele a furaha baada ya kufanikiwa kuingia ndani ya shimo hili, japo kuna giza jingi ila taa gari langu zikanisaidia kuona mbele vizuri sana.Gari za watu wa khalid zikaendelea kunifukuzia kwa nyuma jambo lililo anza kunipa wasiwasi mwingi
“wakinikamata watanila nyama”

Nilijisemea kimoyo moyo, nikamtazama dorecy na kumkuta akiwa bado amepoteza fahamu, upana wabarabara hii iliyo chongwa ndani ya mlima ikazipa upenyo gari za watu wa khalid kutanda njia nzima, huku baadhi ya gari zikijari kunipita ila niliwazui kwa kuwazibia njia kwa mbele.Wakaanza kunipiga risasi kwenye kii cha nyuma cha gari langu, nikazidi kuongeza mwendo wa gari langu, mbaya zaidi barabara hii haina hata kona zaidi ya kunyooka.

Risasi zao nyingi zikafanikiwa kutoboa kioo cha nyuma cha gari na kuzidi kunichanganya akili yangu, nikazidi kukanyaga mafuta hadi mshale wa spidi mita ukagota kwenye spidi ya mwisho ambayo ni mia mbili na hamsini.Nikazidi kwenda mbele, gafla nikakutana na kona ambayo kwa mwendo ambao ninao nikashindwa kukunja na kuisababisha gari kupiga kweney ukuta na kuvunja ukuta huu wa udongo, kufumba na kufumbua nikajikuta gari ikielea hewani, na kuanza kwenda chini kwenye miamba mikubwa ya mawe jambo ambalo lilinifanya niaanze kusali sala yangu ya mwisho kwani, ikitua chini mimi na dorecy wote tutakuwa maiti 
Itaendelea....
 Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!