Tuesday, October 4, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 63 & 64 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Mtunzi : Eddazaria g.MsulwaIlioishia...
Risasi zao nyingi zikafanikiwa kutoboa kioo cha nyuma cha gari na kuzidi kunichanganya akili yangu, nikazidi kukanyaga mafuta hadi mshale wa spidi mita ukagota kwenye spidi ya mwisho ambayo ni mia mbili na hamsini.Nikazidi kwenda mbele, gafla nikakutana na kona ambayo kwa mwendo ambao ninao nikashindwa kukunja na kuisababisha gari kupiga kweney ukuta na kuvunja ukuta huu wa udongo, kufumba na kufumbua nikajikuta gari ikielea hewani, na kuanza kwenda chini kwenye miamba mikubwa ya mawe jambo ambalo lilinifanya niaanze kusali sala yangu ya mwisho kwani, ikitua chini mimi na dorecy wote tutakuwa maiti

Endelea...
Gari ikazidi kwenda chini kwa kasi, gafla nikastukia gari ikiwa imekwama huku, tawi kubwa la mti likiwa limeingia dirishani la nyuma la gari na kuifnya iendelee kuninginia kwenye mti, nikashusha pumzi taratibu huku nikitazama chini, cha kumshukuru mungu, kutoka sehemu tulipo ning’inia hadi chini si mbali sana, nikaufungua mkanda wa gari nilio jifunga, nikamtazama dorecy na kumuoana akiwa anainyanyua nyanyua shingo yake, akizinduka kutoka usingizini.Akanitazama kwa macho yakuchoka 

“eddy”
“nini?’
“yupo wapi khalid?”
“wee mwehu nini, jiulize mwenyewe”
Nilizungumza kwa hasira huku nikiufungua mlango wa gari, kuna tawi lipo karibu na mlango wangu, nikapiga makadirio ya macho na kuona ninaweza kuruka na kulikanyaga pasipo na wasiwasi wa aina yoyote
“eddy unataka kwenda wapi, kwani hapa wapi?”
Dorecy alizungumza huku akitazama chini
“hapa tupo mbinguni mama yangu”
“mbinguni……!!?”
“unauliza tena, hapa ukifungua mlango tuu umeshafika kwa sir god”

Nilizungumza kwa dharau, nikaruka kwenye tawi la mti, kwa bahati nzuri nikatua vizuri na kujiweka sawa mwili wangu, nikashuka kwenye mti taratibu na kufika chini pasipo shida ya aina yoyote, gafla nikasikia kelele za dorecy akiniita jina langu, ikanilazimu nimtazame nikamuona akiwa ananing’inia, huku ameushikilia mlango wa gari uliopo upande wa siti yake
“eddy niokoe mwenziooo, ninakufa mimi”

“ukijiachia tuu unafika mbnguni, hapo tulikuwa kwenye geti la kuingilia mbinguni”
Nilizungumza huku nikimtazama dorecy jinsi anavyo ning’inia huku akiirusha rusha miguu yake hewani
“eddy nakufa mimi”

Dorecy aliendelea kuzungumza kwa sauti ya kilio, huku akiendelea kuning’inia hewani, nikatafuta sehemu yenye jiwe lililo kaa vizuri, nikakaa na kuendelea kumtazama dorecy anaye endelea kuninginia hewani
“eddy niokooe”
“nikuulize kitu dorecy?”
“ehee” alijibu huku akiwa amening’inia
“hivi huku ulifikaje?”
“nikuulize wewe, tumefikaje huku?”

“ahaa unaniuliza mimi tena kwamba tumefikaje huku, unadhani kwamba mimi nilikuwa ni ndege iliyo kufikisha kwenye hii nchi?”
“eddy tuachane na hayo, ninakuomba unisaidiea”
Dorecy alizungumza kwa sauti ya unyong, akiashiria kwamba amechoka sana
“madini yangu yapo wapi?”
“edd siwezi kukujibu hadi nishuke”

“basi wewe si mjeda wa mzee godwin, jishushe mwenyewe”
Nilizungumza huku nikinyanyuka kwenye jiwe, nikiendelea kulichunguza aneo zima la hii sehemu, nilipo hakikisha lipo salama na hakuna uwezekana na watu wa khalid kufika katika sehemu tulipo nikarudi sehemu alipo dorecy akiendelea kuning’inia huku akitoa kilio kwa mbali akilalamika kwamba anakufa

“jiachie”
Nilizungumza huku nikiwa nimesimama chini yake nikimtazama
“ehee?”
“hujasikia, jiachie nitakudaka na hilo jitumbo lako”
“kweli eddy?”
“kama hutaki basi bwana”
“basi najiachia”

Nikaitega mikono yangu usawa wa sehemu anayo ning’inia dorecy, nikahesabu moja hadi tatu, dorecy akajiachia na kutua kwenye mikono yangu, cha kushukuru mungu ametua vizuri kwenye mikono yangu, nikamsimamisha chini na kumuacha akiendelea kuhema kwa nguvu, kama bata mzinga.Nikaanza kupiga hatua za kuondoka katika eneo hili pasipo kusubiria asante ya dorecy huku moyoni mwangu nikijikuta nikianza kusamehe kuhusiana na madini yangu, kwani hakuna uwezekano wowote wa mimi kuyapata kutokana na khalid kujizatiti vizuri katika swala la ulinzi
“edd….Y”

Nilisikia sauti ya dorecy ikiniita kwa unyonge nyuma yangu, nikasimama pasipo kutazama nyuma, nikashusha pumzi nyingi na kugeuka taratibu, nikamuona dorecy akianza kukaa chini taratibu huku akiwa amelishika tumbo lake
“eddy nakufa mimi, tumbo langu”

Dorecy alilalamika huku akiwa amelishika rumbo lake, nikaanza kupata mstuko baada ya kagauni kake ka kulalia alicho kivaa kukiona kikiwa kimelowa kwa damu sehemu zake za siri.Machozi ya uchungu yakaendelea kumtoka dorecy, vilio vya dorecy vikazidi kuongezeka, ikanilazimu kurudi kwa haraka katika sehemu alipo
“eddy mtoto anatoka”

Dorecy alizungumza huku akipanua mapaja yake, wazo la kwanza kunijia kichwani mwangu, ni kukata nguo ya ndani aliyo ivaa dorecy, macho yangu yakaendelea kumtazama dorecy jinsi anavyo toa mayowe ya uchungu
“eddy mwanangu uwiiiiiii”
“yupo wapi?”

Nikastukia kofi zito ikitua kwenye shavu langu, kutoka kwa dorecy ambaye anaonekana kukasirika, macho yake ameyatoa huku jasho jingi likimwagika kutoka na maumivu makali anayo yapata.
“jikaze uzae”

Nilizungumza huku nikiishikilia miguu ya dorecy ambayo ameichanua kwa kiasi fulani, nikaendelea kumuhimiza ajitahidi kumsukuma mtoto, kwani nilisha anza kuona dalili ya majimaji yanayotangulia kabla ya mtoto kuzaliwa.Taratibu nikaanza kuona kichwa cha mtoto kikianza kuchomoza
“push kwa nguvu”(sukuma……)

Nikaendelea kumuhimiza dorecy kwa sauti ya juu, akaendelea kujitahidi kumsukuma mtoto wake atoke nje, nikaiweka mikono yangu karibu na kichwa cha mtoto na kuanza kukipokea kichwa chake taratibu
“endelea mama, mabega yameshaanza kuchomoza”
Hadi mimi mwenyewe jasho likaanza kunitoka kwani si kazi ndogo ya kumzalisha mwanamke
“eddyyyyyyyyyyyyyyyy”

Dorecy alizungumza kwa nguvu, huku akijikamua kwa nguvu zake zote na kumfanya mtoto wake kutoka na kuangukia mikononi mwangu, sikuisikia tena sauti ya dorecy, katoto kake ka kiume, kenye mwili mdogo kakaanza kutoa kimlio kwa mbali, nikajikuta nikifurahi mimi mwenyewe, huku jasho likiendelea kunimwangika uso mzima, nikabaki nikimtazama mtoto huku kitomvu chake kikiwa bado kimeshikana na mama yake, ambaye amepotezafahamu kutokana na maumivu makali ya kujifungua
“huyu mtoto amezaliwa kabla ya siku zake”

Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama mtoto kwani ni mdogo kupindukia, kwa elimu yangu ya sayansi watoto wa aina hii huwa tunawaita njiti kutokana hajatimiza umri halisi wa yeye kuzaliwa kama watoto wengine wanaotimiza miezi tisa

Nikamtazama dorecy kwa macho yaliyo jaa uchovu mwingi, kifua chake kwa mbali kinanyanyuka taratibu na kurudi chini, nikamsogelea na kumtingisha kidogo, ila hakuzinduka
“hichi kitovu kinakatajwe?”

Nilijiuliza swali huku nikikitazama kitovu kilicho ungana kati ya mama na mtoto, nikamuweka vizuri dorecy na kumlaza chali, nikamuweka mtoto wake juu ya tumbo lake kisha nikanyanyuka na kuanza kutafuta ni wapi ninapoweza kupata kitu chenye ncha kali cha kukikata kitomvu cha mtoto, kutokana kumesha pambazuka vuzuri ninaweza kuona kila kitu ambacho kinaweza kuwa chini, nikazunguka aneo la karibu na alipo dorecy ila sikuona kitu kinachoweza kunisaidia kwa muda huu.Ikanilazimu kurudi sehemu nilipo muacha dorecy, macho yangu yakangonana na macho ya chui, ambaye yupo hatua chache kutoka sehemu alipo lala dorecy, ambaye muda wote hajitambui kutokana nakupoteza fahamu
“mungu wangu”

Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama chui ambaye anatoa mingurumo ya chini chini huku akilamba lamba mdomo wake wenye meno makli yenye ncha kali sana, nikachuchumaa chini taratibu pasipo kuyapepesha macho yangu,  nikimtazama chui huyu, nikaokota kipande cha jiwe ambacho nimekikanyanga kwa mguu wangu wa kushoto, kisha nikasimama huku nikiendelea kumtazama chui huyu
“shiiiii”

Nilitoa mlio huo, nikimfukuza chuki huyu ambaye taratibua alichaanza kupiga hatua za kumfwata dorecy na mwanaye katka sehemu ambayo wamelala chini, chui akasita kidogo na kunitazama kwa macho yake makali
“toka opo”

Niliendelea kuzungumza huku nikimtishia kwa jiwe ambalo nimelishika mkononi mwangu, mwili mzima ukaanza kunitetemeka baada ya chui kubadilisha muelekeo wake na kuanza kunifwata mimi kwa mwendo wa madaha katika sehemu ambayo nimesimama, kikataka kupiga hatua moja nyuma, gafla nikajikuta nikianguka chini kama mzigo, kitendo cha kujaribu kunyanyuka tayari chui amenirukia kifuani kwangu, kichu cha kwanza kukiwahi katika kukishika ni shingo yake, nikakizuia kichwa chenye mdomo wake ulio jaa meno makali, usinidhuru kwenye mwili sura yangu, 

Chui huyu akaendelea kunikwaruza na kucha zake, sehemu mbali mbali za mwili wangu, huku akijitahidi kuushusha mdomo wake kuing’ofoa pua yangu, nikaendelea kujikaza kwa juhudi zangu zote, uzito wa chui huyu ni mara mbili ya uzito alio nao mke wangu phidaya, mikono yangu ikaanza kutetemeka kwa kuchoka, huku taratibi nikiendelea kujikaza kizuia shingo ya chui huyu.
“mungu wangu nisaidie mimi”

Niliendelea kuzungumza, huku mikono ikianza kuchuka taratibu chini, ikizidiwa uzito na kichwa cha chui huyu anaye onekana ananjaa kali, sikujali jinsi anavyo nikwaruza sehemu za mwili wangu kwa kutumia miguu yake ya nyuma na yambele yenye kucha kali sana, kikubwa ni kujitolea maisha yangu kwa ajili ya dorecy na mwanaye niliye mzalisha
“siwezi kufa kijinga”

Nikaanza kujitutumua kiume, huku nikiipandisha mikono yangu juu nikijitahidi kumtoa chui huyu mwilini wangu, juhudi na nguvu zangu taratibu zikaanza kuzaa matunda, kwani nikafanikiwa kumgeuza chui na kumuegemesha kando.Mwili wangu mzima unavuja damu kataika sehemua alizo nikwaruza chui huyu, mikono yangu sikuiruhusu kutoka mikononi mwa chui huyu.Nikaanza kukidundiza kichwa chake chini, kwenye jiwe kubwa.Chui akazidi kupandisha hasira na kutoa pumzi kali iliyo anza kuyafanya macho yangu kumwagika machozi mithili ya mtu aliye pigwa bomu la machozi na askari wa kutulizaghasia
“eddyyy”

Niliisikia sauti ya dorecy ikiita kutoka katika sehemu alipo lala, nikageuza shingo yangu kumtazama sehemu alipo, nikamuona amekaa chini huku amemshika mwanaye, kitendo cha mimi kumtazama dorecy kikawa ni kosa kubwa kwangu kwani chui, akanibinua kwa nguvu zake zote akaanza kunikwaruza huku meno yake akijaribu kuyakita kwenye paja langu la mguu wa kulia.Maumivu yasiyo na kifani yakaanza kuutesa mguu wangu, machozi ya uchungu yakanimwagika.Nikaokot kipande cha jiwe lilicho chongoka na kuanza kumkita nacho chui cha kichwani mwake

Chui akazidi kuyakita meno yake kwenye paja langu, nia yake kuu ikiwa ni kunikata mguu wangu, nikazidisha kumbabiza kwa jiwe langu nililo lishika, kelele za maumivu zikaniendana na kasi yangu ya kukikita kicha cha chui kwa ncha ya kipande cha jiwe, kichwa cha chui kikaanza kufumuka damu huku fuvu lake la kichwa likipasuka na ubongo wake kutoka nje, ikawa ni mwisho wa maisha yake
“ahaaaa”

Nilizungumza huku nikilia kwa uchungu mkali, nikaushika mdomo wa chui na kikauachanisha mdomo wake wenye meno yaliyo kita kwenye paja langu, japo maumivu ni makali sana ila nikajitahidi hivyo hivyo hadi paja langu nikalitoa kwenye kinywa cha chui na kujilaza pembeni,nikamtazama dorecy sehemu aliyo kaa nikamuona akijitahidi kusota kuja sehemu niliyo jilaza mimi, huku sura yake ikiwa imejaa machozi mengi
“usije”

Nilizungumza kwa sauti iliyo kwaruza sana huku nikimnyooshea mkono asifike katika sehemu nilipo mimi, nikajinyanyua taratibu huku damu zikendelea kuvuja kwenye paja langu.Chakumshukuru mungu, chui huyu meno yake, hayakufanikiwa kukutana na kutoa kipande cha nyama kwenye paja langu, au kuukata kabisa mguu wangu, nikaanza kutembea huku nikiuburuza mguu wangu ulio jeruhiwa hadi nikafika sehemu alipo kaa dorecy
“mtoto yupo hai?”

Nilimuuliza dorecy huku nikimtazama mtoto wake aliye yafumba macho yake
“ndio”
“ohhh asante mungu”
Nilizungumza kwa sauti ya kukwaruza sana huku damu zikiendelea kunimwagika mwilini mwangu, machozi yafuraha yaliyo changanyikana na uchungu yakaendelea kunitiririka usoni mwangu

“eddy ninakupenda sana, samahani kwa yale yote niliyo kufanyia, ninaamini kwamba mimi ni binadamu ninaye weza kuhadaika kwa vitu vidogo sana.Sikustahili unisaidie, ilikuwa ni haki yangu kutafunwa na huyo chui mimi na mwanangu, ila wewe uliweza kujitolea maisha yako kwa ajliya yangu na mwanangu”
Dorecy alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, nikamtazama kwa muda jinsi anavyo endelea kulia kwa uchungu sana

“usilie, nimekusamehe muda mwingi sana, hali yangu inazidi kuwa mbaya na hapa niporini, ninjua sinto weza kutoka nikiwa hai, kifo kitakuwa juu yangu, ninakuomba umtafute msichana mmoja anaitwa phidaya, anamimba yangu nakuomba unisaidie kwa hilo pale nitakapo kuwa nimeshakufa”
“hapana eddy, huwezi kufa nakuomba usizungumze hivyo”
“dorecy, damu nyingi inanitoka nilazima….”
“edddyyuuu tazama nyuma yako”

Sauti kali ya dorecy ikaniomba kugeuka nyuma na mimi nikafanya kama alivyo niambia, ila tayari nimeshachelewa risasi mbili kutoka kwa watu wa khalid waliofika kwenye eneo hili, zikatua kifuani mwangu, na taratibu nikaanza kwenda chini, nikapiga magoti na kumtazama dorecy, aliye yatoa macho yake huku akishangaa, kuto kuamini kitu anacho kiona

“bye….”
Nikaanguka chini, huku nikilalia tumbo na giza nene taratibu likaanza kuyafunika macho yangu, na kwambali nikaanza kuisikia sauti ya dorecy ikiliita jina langu kwa uchungu

                           *****sory madam*****(64)

“bye….”
Nikaanguka chini, huku nikilalia tumbo na giza nene taratibu likaanza kuyafunika macho yangu, na kwambali nikaanza kuisikia sauti ya dorecy ikiliita jina langu kwa uchungu
Endelea
Sikuweza kusikia kitu chochote kinacho endelea kwenye masikio yangu
                                                                                               
Kwa mbali nikaanza kuhisi sauti za watu wakizungumza taratibu, nikajaribu kuyafumbua macho yangu kutazama ili nione ni kina nani, ila ukungu mwingi uliojaa machoni mwangu sikuweza kuwaona vizuri.
“eddy”

Nilisikia sauti ikiniita masikioni mwangu, ambayo inaendana na sauti ya mke wangu phidaya, nikageuza shingo yangu kutazama sehemu inapo tokea sauti hiyo, nikawaona watu wawili wakiwa wamesimama huku mmoja akiwa amevalia mavazi meupe huku wapili nguo zake zikiwa na rangi mchangayiko.

“eddy mume wangu upo salama?”
Sauti ya phidaya ikaendelea kupenya masikioni mwangu, nikajaribu kuzungumza ila kinywa changu nikakikuta kikiwa ni kizito sana, nikabaki nikimtazama phidaya mke wangu, aliye valia gauni lenye rangi machanganyiko, mkono wa pihidaya ukapita kwenye sura yangu, kisha mwanaume aliye valia nguo nyeupe akamshika na kumuondoa ndani ya chumba

Hali yangu ya afya ikazidi kuhimarika siku hadi siku, nikiendelea kupatiwa huduma na madaktari ambao sikuwafahamu, zikapita siku kadhaa nikiwa kitandani nikiendelea kuuguza majeraha yangu ya mwili mzima huku phidaya akija kunitembelea kila siku, ila kitu kikubwa ambacho ananificha ni jinsi ya mimi kufika katika hospitali hii
“baby ngoja mimi nirudi hotelin”

Phidaya alinyanyuka kiuvivu huku tumbo lake likiwa kubwa kiasi, kutokana na ujauzito wake alio kuwa nao
“ngoja kwanza”
Nilimuambia phidaya huku nikimshika mkono wake wa kushoto, uliokuwa karibu yangu
“kwa nini huniambii ukweli, juu ya kufika kwangu hapa”
“eddy nilisha kueleza kwamba, nitakujibu mume wangu siku ukiwa umepona vizuri, hili swala halina haja ya wewe kulijua kwa wakati huu

“hata kama, kwani kukuuliza jinsi ya mimi kufika hapa imekuwa ni shida, si ndio?”
“hapana mume wangu, ila kikubwa ni wewe afya yako kuwa katika hali ya uzima”
“powa kama hutaki kuniambia chochote ninakuomba uende zako”

Nilizungumza kwa hasir huku nikimtazama phidaya aliye simama pembeni ya kitanda changu,
“baby umekasirika?”
“hapana, wewe nenda”
Phidaya akaanza kupiga hatua za kuondoka kuelekea ulipo mlango wa kutokea katika chumba cha hospitalini, kabla hajaufikia nikamstua
“na usipo nikuta, usijilaumu”

Ikamlazimu phidaya kugeuka na kunitazama kwa macho ya mshangao mwingi, taratibu akarudi na kukaaa kwenye kiti, huku sura yake ikiwa na huzuni kidogo
“mume wangu ni kwanini unazungumza maneno kama hayo, unajua ni jinsi gani unavyo utesa moyo wangu”
“tatizo sio kuutesa moyo wako ila tatizo ni kwanini hutaki kuniambia ukweli juu kufika kwangu hapa, kwa mtazamo wangu hapa si iraq, siwezi kuendelea kukaa sehemu ambayo siijui ni wapi nikifa j…?”
“eddy inatosha…”

Phidaya alinikatisha na kuzungumza kwa sauti kubwa ya ukali huku machozi yakimwagika usoni mwake, akanitazama na macho yake makubwa kiasi ambayo tayari yalisha anza kubadilika rangi na kuwa mekundu kiasi
“eddy unajua ni jinsi gani, tabu niliyo ipata hadi kukuleta hapa eheeeee? Ulikuwa ni mfu wewe usiye jitambua, umeyafanya maisha yangu kuwa ni yakuwindwa kama kitu cha thamani kwa ajili yako”

Phidaya alizungumza kwa sauti ya ukali iliyo jaa hasira
“utaka kujua kwamba hapa ni wapi si ndio?”
Swali la phidaya likaniacha mdomo wazi huku nikishindwa kujua ni jinsi gani nimjibu
“si unataka kujua, mbona uzungumzi?”
“ndio”
Nilijibu kwa unyonge baada ya kumuona phidaya akinijia juu
“hapa manila, philipines”
“ndio wapi?”
“ndio hapa”

Phidaya alinijibu kwa ufupi huku akinitazama machoni, akanyanyuka na kupiga hatua za haraka hadi shemeu ulipo mlango akafungua na kutoka, nikajikuta nikishusha pumzi nyingi, huku nikuutazama mlango aliotoka phidaya.Kitu kikubwa ambacho kunaniumiza kichwa ni juu ya kwanini phidaya hataki kunieleza ukweli jinsi ya yeye alivyo fika hapa
Siku mbili zikapita pasipo kumuona phidaya, jambo lililoanza kuzua wingi wa maswali kichwani mwangu, huku nikijiuliza ni nikwanini sijkumbili hizi hajatokea.

“au hao watu wanao muwinda ndio wamemteka?”
Niswali jingine lililotokea kuniumiza kichwa change, kutokana nimeshaanza kuruhusiwa kutoka nje ya maeneo ya hii hospitali iliyojaa watu wenye asili ya bara la ulaya na asia.Sikuwa na rafiki zaidi ya kuzunguka kila eneo la hospitali huku nikiwa nimevalia nguo nyeupe zinazo fanana na wangonjwa wengine wanao zunguka zunguka katika eneo hili la hospitlini

Baada ya kuhisi kuchoka nikaamua kurudi kwenye chumba change, kabla sijakifikia nikawaona jamaa wawili walio walia nguo nyeusi pamoja na miwani wakiingia ndani ya chumba change, ikanilazimu kujibanza kwenye moja ya kona ya ukuta kutazama kujua ni kitu gani amacho kitaendelea, baada ya dakika kama tatu hivi jamaa wakatoka na kuondoka, jambo lililo anza kunipa mashaka mengi
“niende au nisiende?”

Nilijiuliza huku mwili mzima ukinitetemeka, nikatazama mlango wa chumba changu kisha nikajipa matumaini mimi mwenye kwamba hakuna kitu kibaya kitakacho tokea juu yangu, nikaanza kupiga hatau za kwenda kilipo chumba change, nikafika kwenye mlango na kukishika kitasa, nikashusha pumzi na kufungua mlango taratibu.Nikamkuta phidaya akiwa amekaa kwenye kiti pamoja na mwanamke aliye valia baibui jeusi, huku usoni mwake akiwa amejiziba na kubakisha macho yake, nikawatazama kwa muda huku nao wakinitazama, msichana aliye vaa baibui akajifungua uso wake na kujua kwamba ni dorecy

“mbona unashangaa?”
Dorecy aliniuliza huku akinyanyuka kwenye kiti nilicho kikalia
“hapana”
“karibu ndani ukae”
Nikapitiliza moja kwa moja na kukaa kitandani mwangu, na kuwatazama phidaya, aliye nunu na dorecy ambaye sura yake ipo kawaida tu
“ninafuraha kukuona tena ukiwa hai eddy”
“asante”

“niliwaagiza watu wangu wakakutafute huko nje, kutoka tulilkuja muda mrefu hatukuona, ila tulivyo wauliza manesi wakadai kwamba upo kwenye maeneo ya viwanja vya michezo”
Dorecy aliendelea kuzungumza huku akiwa amesimama akinitazama kitandani sehemu nilipo kaa
“ila vipi bado unamaumivu ya vidonda vya risasi?”
“hapana vimesha kauka”

Ukimya ukatawala ndani ya chumba huku kila mmoja akiwa yupo kimya akimtazama mwenzake aanze kuzngumza.Phidaya akasimama na kutaka kutoka ndani ya chumba ila dorecy akamkamata mkono
“shoga yangu ninakuomba utulize hsira usiondoke”
“sioni sababu ya mimi kuendelea kukaa hapa”
“ndio ninatambua ya kwamba unahasira sana, ila ninakuomba utulie kwani kuendelea kuwa na hasira haitasaidia kupatana kwenu”

Dorecy aliendelea kuzungumza huku akiwa ameushika mkono wa phidaya aliye vimba kwa hasira, sikujua ni kitu gani ambacho kimemkasirisha phidaya hadi ikafikia hatua ya yeye kunichukia kupita maelezo.Phidaya akarudi na kukaa kwenye kiti chake alichokuwa ameka
“eddy natambua ya kwamba hujui ni kitu gani ambacho kinaendelea kwa wakati huu, ila utaelewa tuu”
“kwani mke wangu unatatizo gani?”
“nani mke wako?”
“haaaa”

Ilinibidi kushangaa tu kwani sikulitarajia jibu kama hili la phidaya kunijibu mimi, kwaishara dorecy akaniomba ninyamaze kimya kwamaana ananijua mimi vizuri sana pale ninapokuwa nimekasirika
“eddy ile siku ambayo ulipigwa risasi kule porini, mume wangu alinichukua mimi pamoja na mtoto, akiamini kwamba wewe umeshafariki.Walinipeleka hadi nyumbani, ila kwa siri sana nilizungumza na hawa walinzi wangu wawili nilio kuja nao huku”

“walienda kukuchukua kule porini nakunipele kwenye moja ya hospitali pasipo khalid kugundua kitu cha aina yoyote.Kwa kipindi chote ulipokuwa kwenye hospitali ya siri, ukifanyiwa matibabu ya kuyaokoa maisha yako, niliendelea kulifanyia kazi ombi lako la wewe kumtafuta mke wako, hadi nikafanikiwa kimpata”

Tulinyamaza kimya mimi na phidaya tukimuacha dorecy akizungumza,
“baada ya kukutana na bibie hapa, nilimueleza kila kitu juu yako, na maisha yetu ya nyuma, kitu ambacho sikukijua ni kwamba kunabadhi ya mambo ambayo wewe hukumuadisia mkeo na mimi nikajikuta nikumuadisi”

“phidaya alikasirika sana, na kukiri kwamba hakufahamu wewe, ila nileiendele kumbembeleza ili asifikie hatua ya kukutenga wewe, nashukuru mungu kwamba alinielewa, kumbe kunakipindi kunatukio ambalo mulilifana wewe na yeye, ambalo kule iraq hadi leo munatafutwa na serikali ya kule”

“ngoja kwanza, tukio la mimi kutoroshwa hospitali ndilo lilolofanya sisi kutafutwa?”
Nilimuuliza dorecy na kumfanya phidaya kunitazama kwa jicho kali lililo jaa hasira
“ndio, ila kuna ishu khalid alitaka kukufanyia wewe na phidaya akaiingilia kati na kuwa adui namba mwengine wa khalid”
“jambo gani hilo?”
Hata kabla dorecy hajanijibu tukasikia milio mingi ya risasi kwenye kordo yetu huku kelele za watu wagonjwa na manesi wakike zikisikia jambo lililo tustua sote ndani ya chumba

  Itaendelea...

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!