Friday, October 7, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 65 & 66 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilioishia
Nilimuuliza dorecy na kumfanya phidaya kunitazama kwa jicho kali lililo jaa hasira
“ndio, ila kuna ishu khalid alitaka kukufanyia wewe na phidaya akaiingilia kati na kuwa adui mwengine wa khalid”
“jambo gani hilo?”
Hata kabla dorecy hajanijibu tukasikia milio mingi ya risasi kwenye kordo yetu huku kelele za watu wagonjwa na manesi wakike zikisikia jambo lililo tushtua sote ndani ya chumba

Endelea
Milio ya risasi ikaendelea kurindima nje ya chumba tulichopo na kuzidi kutupagawisha sote tuliopo ndani ya chumb hichi, wasiwasi mwingi ukawa kwa dorecy ambaye fika anaoenekana kuchanganyikiwa
“eddy hao ni watu wa mume wangu”
Dorecy alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka, nikapiga hatua za haraka hadi dirishani na kuchungulia chini ambapo kuna umbali wa ghorofa mbili kwenda chini.
“hatuwezi kutoka humu ndani”
Nilizungumza huku nikiwatazama dorery na phidaya
“itakuwaje sasa?”
 
Phidaya alizungumza huku machozi yakimwagika kwa wingi.Nikapiga hatua hadi mlangoni, nikachungulia kwenye sehemu ya kuingizia funguo, nikamshuhudia jamaa mmoja akitandika risasi ya kichwa mzee mmoja aliye ambiwa alale chini ila akaleta kiherehe cha kujinyanyua, ndipo akakutana na maafa hayo ambayo ni yakinyama sana.
 
Gafla simu ya phidaya ikaita na kutufanya sote kumgeukia na kumtazama kwa macho ya mshangao, kwa kiwewe alicho nacho akashindwa hata kuikata na kujikuta akiiachia na kuanguka chini, nikachungulia tena kwenye tobo la kuingizia funguo na kumuona jamaa aliye muua mzee, akiutazama mlango wetu kwa umakini.
“ingieni bafuni”
 
Nilizungumza kwa sauti ya chinichini, dorecy akamshika mkono phidaya na kukimbilia kwenye bafu liilopo humu ndani ya chumba changu.Jamaa akapiga hatua hadi ulipo mlango uku bunduki yake aina ya ‘short gun’ ikiwa mkononi mwake.

Nikajibanza nyuma ya mlango, huku mapigo ya moyo yakinienda mbio kiasi kwani bado sijaiamini afya yangu kwa kiasi kikubwa kutokana na majeraha ya risasi yaliyopo mwilini mwangu.Mlango taratibu ukafunguliwa, nikaanza kuona kiatu cheusi kikitangulia mbele, jamaa akasimama kwa muda, gafla simu ya phidaya iliyo anguka chini ikaanza kuita tena na kumfanya jamaa kupiga hatua za taratibu hadi sehemu ilipo anguka simu na kuiokota.Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio, kwani endapo jamaa atageuka nyuma nilazima ataniona.Akaitazama simu ya phidaya kwa muda na kuitupa chini na kuchanguka, akatazama mlango wa kuingilia bafuni ambapo ndani yake yupo phidaya na dorecy
 
Simu ya jamaa ikaita, akaitoa kwenye koti lake, akaipokea nakuiweka sikioni mwake, akazungumza kwa lugha ya kiarabu, nikastukia kumuona jamaa akichomoka kwa kasi, ndani ya chumba pasipo kuniona nyuma ya mlango, ving’ora vya gari za polisi, nikaanza kuvisikia na kunifanya nishushe pumzi nyingi, na kujikalia chini, huku jasho jingi likimwagika.Ndani ya dakika kadaa askari kadhaa wakawa wameingia katika sehemu tulipo, dorecy na phidaya wakatoka bafuni, askari na madaktari walio salimika katika vamizi la majambazi hawa
                                                                                                  ***
Wagonjwa tulio salimika tukahamishwa kwenye hospitali moja, inayo milikiwa na jeshi la nchi ya philipines, matiibabu yangu hayakuchukua muda mrefu sana, nikaruhusiwa kutoka hospitalini na kuhamia kwenye hoteli ambayo phidaya anaishi kwa siri sana, na amelipiwa gharama zote na dorecy ambaye tayari amerudi kwa mume wake.
“phidaya,itatubidi turudi tanzania”
 
Nilizungumza huku macho yangu yakimtazama phidaya aliye jilalia kiuvivu kwenye kitanda, huku akiwa tumbo wazi akilichezea chezea kwa kiganja chake tumbo lake lenye kiumbe ndani
“si usubiri niweze kujifungua kwanza”
“hatuwezi kuishi hapa, pasipo sisi kuwa na kazi, unadhani tutayamudu vipi haya maisha?”
“sawa mume wangu, je tukirudi huko tanzania, tutafikia wapi wakati umesha sema kwamba mama yako alitekwa na baba yako mkubwa”
 
Nikamtazama phidaya kwa muda, kwani kitu alicho kizungumza kinamaana kubwa sana kwangu, isitoshe sijajua ni hali gani inayo endela kati ya mzee godwin na mama yangu.Nikanyanyuka taratibu na kuisogelea computer iliyopo kwenye meza humu chumbani kwetu, ambayo imeunganishwa na huduma ya internet.Nikaiwasha taratibu, baada ya muda nikafungua mtandao wa google
“unataka kufanya nini?” phidaya alizungumza huku akipiga hatua na kuja kukaa kwenye kiti nilicho kikalia mimi
“kuna mtu nataka kumtafuta”
“nani?”
“baba yangu mzazi, anaishi afrika kusini”
“mmmm sawa”
 
Nikaliingiza jina la baba yangu mzazi kwenye sehemu ya kutafutia, kwenye mtandao huu ambao unasadikika ndio mtandao mkubwa duniani kote, ulio kusanya mambo mengi sana, ndani ya sekunde kadhaa nikawa nimefanikiwa kulipata jina la baba yangu mzazi pamoja na historia yake, cha kumshukuru mungu nikakutana na taarifa nyingine iliyo nipendezesha moyoni mwangu, kwani ameingia kwenye orodha ya matajiri kumi nchini afrika kusini huku yeye akiwa nafasi ya nne kutoka juu.
“inabidi twende nyumba ni kwa baba”
“sawa mume wangu”
 
Phidaya hakuwa na pingamizi na maamuzi yangu niliyo yachukua, nikaanza kufwatilia hati za kusafiria kuelekea afrika kusini, kutuokana na pesa ambazo dorecy anatusaidia, sikupata tabu sana katika kukamilisha maswala usafiri wa ndege.Siku ya pili tukakusanya kila kitu kilicho chetu kwenye hoteli ambayo tunaishi, tukakodi tanksi hadi uwanja wa ndege, muda wa kupanda ndege ulipo wadia, tukaungana na wasafiri wengine na kuingia ndani ya ndege, na taratibu safari ikaanza, huku moyoni mwangu nikimuomba mungu atufikieshe salama, kwani kumbukumbu za ajali iliyo tokea nchini kenya kipindi nikitokea afrika kusini, inaendelea kuzunguka ndani ya kichwa changu kama mkanda wa filamu.Phidaya kwa kudeka muda wote kichwa cheka amekilaza kifuani mwangu, huku akiimba nyimbo za kunibembeleza kwa sauti ya chini
“baby” nilimuita kwa sauti ya upole
“mmmmm”
 
“naomba niende msalani”
“sawa, ila usichelewe mume wangu”
Phidaya alinijibu taratibu huku akijinyanyua, kifuani kwangu taratibu, nikasimama, na kuanza kupiga hatua za kuelekea chooni, nikaingia ndani ya choo na kumaliza haja zangu zote, nikanawa uso wangu ili kuutoa uchovu na usingizi unao ninyemelea usoni mwangu.Nikafungua mlango, gafla nikastulia kitu chenye ncha kali kikinikita mgongoni mwangu, na sauti ikasikika kutoka nyuma yangu
“tulia kama ulivyo upo chini ya ulinzi, mr eddy”
 
 *****Sorry Madam*****(66)

Mwili ukanisisimka na kujikuta nikitulia kimya, huku kwa mbali mapigo ya moyo yakianza kunienda mbio, ila sauti niliyo isikia nyuma yangu haikuwa ngeni masikioni mwangu, nikatamani kugeuka na kutazama nyuma ila sikuwa na uwezo kutokana nipo chini ya ulinzi wa mtu huyu.
“oya wewe bwege kweli, kijiko pia kinakutisha”
 
Mtu aliye nyuma yangu alizungumza huku akizunguka na kuja mbele yangu, macho yangu yakakutana na john, rafiki yangu wamuda mrefu tangu tukiwa shule ya sekondari, akiwa amevalia mavazi maalumu kama watumishi waliopo kwenye hii ndege, nikashusha pumzi nyingi na kubaki tukitazamana.Tabasamu likatawala usoni mwa john na mimi pia nikajikuta nikitabasamu na kukumbatiana naye huku tukipigana pigna migongoni kwani, nimiaka kadhaa imepita pasipo sisi kuonana
 
“eddy mwanangu, aahaa nikitambo sanaa”
Johna alizungumza kwafuraha huku tukiachiana
“kweli mwanangu, haya mbona huku tena kwenye ndege?”
“ndugu wee acha tuu, maisha mwanangu yanabadilika”
“ndipo unapofanyia kazi?”
“nipo training(mafunzo), napata pata ujuzi”
“pcb wewe umekuwaje, umekuja kwenye ndege huku, au ndio hiyo elimu ya tanzania, hkl anakuwa mkaguzi wa fedha, wakati mathematics amenyoosha mswaki?”
Nilizungumza kwa utani huku nikiwa nafuraha usoni mwangu
“ahaaa kaka, ndio maana yake, huku tumeingia hivyohivyo tuu, tena kwa masaada wa mama yako ndipo aliniunganisha huku”
 
Taarifa ya john ikanistua kidogo nakujikuta nikaanza kumfkiria mama yangu
“mama yangu yupi?”
“haaa kwani eddy wewe una mama gani mwengine?”
“hapana nimekuuliza hivyo kutokana nina maana yangu?”
“mama yako ambaye kwa sasa ni waziri wa usafirishaji, ametoka kwenye kitengo cha afya”
“unataka kuniambia kwamba mama yangu yupo hai?”
“ndio yupo hai, tena yeye anakutafuta wewe”
“john umeniacha njia panda hemb……..”
Sikuimalizia sentesi yangu, msichana mmoja aliye valia mavazi kama john, alimuita john kwakutumia lugha ya kingereza
“am coming”(ninakuja)
John alimjibu msichana aliye muita huku akimtazama usoni mwake
“sasa eddy, ngoja mimi nikaendelee na majukumu ndugu yangu”
 
“sawa ila kaka nahitaji tuzugumze zaidi”
“usijali kwani wewe unaelekea wapi?”
“afrika kusini, kwa mzee”
“mzee gani tena, kwa maana baba yako amefungwa?”
“eheee”
“kwani eddy ulikuwa wapi siku zote”
“john”
Sauti ya msichana aliye muita john mara ya kwanza ilisikika tena, ikimuita kwa msisitizo
“kaka baadaye”
John aliondoka kwa kupiga hatua za haraka kwenda katika sehemu alipo itwa, nikashusha pumzi kwa mara nyingine, huku kichwa changu kikiingia mawazo mapya katika maisha, kwani kwakipindi hichi, nilichokaa mbali na nchi yangu sikujua ni mambo yapi yaliyo endelea kwenye nchi yangu, na pia sikujua ni kitu gani lilichotokea kati ya mama yangu na mzee godwin, baba yangu mkubwa ambaye kwa mara ya kwanzi nilidhani kwamba ni baba yangu mzazi.Nikarudi kwenye siti yangu, huku nikiwa nafuraha usoni mwangu
“mbona umechelewa kurudi ulikuwa na nani?”
 
Phidaya aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu, nikajikuta nikitabasamu kwa furaha na kumtazaka usoni mwake
“mke wangu, ninafuraha wee acha tuu”
“furaha gani tene hiyo?”
“kwanza nimekutana na rafiki yangu wa kipindi kirefu sana”
“nani?”
“nitakuambia tukitulia”
“ahaaa eheee, sawa bwana”
Phidaya alizungumza kwasauti yakudeka huku akigeukia uapande wapili wa siti yake, nikaupitisha mkono wangu mmoja kwenye kiuno chake na kumvuta karibu yangu na kichwa chake akakilaza kifuani kwangu taratibu
“umekasirika?”
“ndio”
“nisamehe mke wangu”
 
“sikusamehe, hadi uniambie umekutana na nani?”
Nikamuadisia phdiaya, historia fupi kati yangu na john, nikamuelezea kuhusiana na maisha ya mama yangu japo hakunieleza kwa undani, sana kuhusiana na maisha yaliyo jitokeza kwenye familia yangu ila moyoni mwangu kidogo nikipata matumaini yakumuona mama yangu, hadi namaliza kumuadisia phidaya, mwenzangu tayari usingizi umepitia nakulala fofofo.Baada yamasaa kadhaa, sauti ya msichana ilisikika kwenye vipaza sauti vilivyomo ndani ya ndege, akituomba tufunge mikanda kwani ndege ipo karibuni kutua katika uwanja wa ndege wa ‘johannesburg’.Ndani ya dakika kadhaa ndege ikatua kwenye uwanja  na abiria wakaanza kushuka mmoja baada ya mwengine, john akafika hadi kwenye siti yetu, ambapo ametukuta tunatoa toa mabegi yetu katika sehemu ambayo tumeyaweka
“huyu ndio, john ambaye nilikuwa nikikuambia”
Nilimtambulisha john kwa phidaya
“john huyu ni mke wangu, anaitwa phidaya”
“ahaaaa, habari yako shemeji”
 
Phidaya na john wakasalimiana kwa muda huku wote wakiwa wanafuraha, john akatuomba tumsubiri nje ya uwanja, yeye nawezake wakimalizia hatua za makabidhiano ya ndege, nawahudumu wengine ambaoa watarudi kwenye safari ya mzunguko wa ndege hiyo.Tukakaguliwa mimi pamoja na mke wangu phidaya, tukatoka nje ya uwanja wa ndege na kutafuta sehemu yakukaa, ndani ya dakika kumi na tano john akaja katika sehemu tuliyo kaa, kutokana ipo wazi sana kwa watu kutuona
“jamani, sijui nyinyi wezangu munaelekea wapi?” jonh alituuliza
“sisi tunasafari yakuelekea kwenye cap town”
“munaonaje tukafikizia hotelin leo, kisha kesho muweze kwenda kwakutumia usafiri watreni za umeme”
 
John alitushauri, sikuwa nakipingamizi kutokana hatukumaliza mazungumzo na john juu yakitu ambacho kimetokea kwenye maisha ya miaka michache iliyo pita, tukakidisha taksi iliyotupeleka kwenye hoteli moja iitwayo ‘mondior concorder’ iliyopo pembezoni mwa barabara ya albetina sisulu, tukafanikiwa kupata vyumba viwili vyenye hadhi nzuri kwawageni kulala
“baby mimi najisikia kuchoka, nitapumzika zangu ndani”
Phidaya alizungumza mara baada ya kuingia katika chumba tulicho chukua
“kwanini?”
“ kuna chakwanini wakati nimekuambia kwamba nimechoka, hivi unadhani hili jitoto lako humu ndani halinichoshi?”
“mmmm mke wangu na wewe kwakudeka, haujambo”
“nini”
“yaishe mama kijacho”
“wewe niudhi tuu”
Phidaya alizungumza huku akijilaza kitandani taratibu, kwa jinsi mwili wa phidaya ulivyo umbika, umekuwa nikivutio kizuri kwangu ambacho sichoki kikitazama kila muda na dakika zake zinavyo zidi kukatika
 
“kweli hapa nimepata mke”
Nilijisememea kwasauti yachini chini, nakumfanya phidaya kunitazama kwamacho makali, akaachia msunyo mkali na kujiweka vizuri kitandani, kutoka tayari kumeshaanza kupambazuka, sikuona haja ya mimi kuendelea kulala kitandani, kusimama kwenye dirisha la chumbani chetu lenye kioo kikubwa, na kuaanza kuuangalia mji huu jinsi ulivyo jengeka kwa majengo yaliopo kwenye mpangilio mzuri
“huji kulala hapo umesimama kama mshumaa wapasaka, maana yake ni nini?”
 
Phidaya alizungumza huku akitumbulia macho yake, makubwa kiasi
“mke wangu saa hizi, saa kumi na mbili na nusu, nitalala nini?”
Phidaya akajifunika kwashuka gubigubi, kwa jinsi ujauzito wa mke wangu ulipo fikia, unampelekesha kama mtoto mdogo kwani kila analo lifanya nikituko kwangu.Asubuhi namapema nikakutana na john kwenye mgahawa uliopo chini ya hoteli hii, akaanza kuniadisia kila kitu amcho kilitokea kwapindi kizima nilipokuwa sipo nchini tanzania
“mama, yupo salama kabisa na nijuzi kati tu, hapa nilikuwa naye kwenye ndege yetu inayo elekea tanzania, alikuja huku kwa mambo yake binafsi”
 
“ehee ilikuwaje?”
“siku ambayo ilikuwa ni graduation(mahafali) yakumaliza kidato cha sita ndipo, siku ambayo nilikutana na mama wakati wausiku.Ile siku nakumbuka ilikuwa nijumamosi, wakati wausiku nilikuwa na demu mmoja sidhani kama utakuwa unamfahamu”
“alikuwa ni mwanafunzi?”
“ndio, anaitwa catherina?”
“simkumbuki”
“nahisi alihamia kipindi wewe, umeshaondoka, kama unavyojua mwanangu maisha ya shule, tuliamua usiku kwenda sehemu yakujificha kule msituni, ambapo tulianza, kufanya yetu kwenye kichaka”
 
“mmmm, hukuwa na pesa ya chumba nini?”
“ahaaa hoteli zote zilijaa wageni, waliokuja kwenye sherehe, kipindi tunafanya yetu, kwa mbali tulianza kusikia vishindo vya watu wakitembea kwenye eneo tulilopo, ikatulazimu kukatisha mautamu yetu, nakujikuta tukijificha kwenye kichaka chetu”
“tuliwashuhudia watu hao wakiitupa miili ya watu wawili, huku wote wakibishana nakudai kwamba watu hao tayari wameshafariki, walipo watupa, wakaondoka zao na kutuacha sisi, tukiwa tunatetemeka”
“sasa mulikuwa munatetemeka nini?”
“weee, eddy wewe unazungumza tuu, kukutana na watu kama wale si kitu kidogo, mbona catherina alijikojolea kwa woga”
 
“dooooo” nilijikuta nikicheka
“sijui hata ujasiri niliupatia wapi, nikajikuta nikipiga hatua za kwenda kutazama sehemu walipo tupwa watu wale, japo catherina alikuwa na wasiwasi, kufika ile sehemu, nikastukia kuona mmoja wao akistuka na kutoa ukelee, kumcheki vizuri wapili naye nikagundua kwamba yupo hai, ambaye ni mama yako, ila miili yao ilikuwa imedhohofika sana, tena sana, ilinilazimu kwenda kumuomba, lucas gari lao”
“lucas nani?”
“lucas martin, tuye jamaa wa hkl aliyekuwa anajisikia sana”
“ahaaa nimemkumbuka”
 
“alikuwa anatembeala na gari ya baba yake, aliyokuja nayo kwenye mahafali, basi tuliwapeleka kwa bibi yangu aliyepo pale pela arusha yeye ni nesi, ila nilifanya nisiri sana watu wasijue kutokana mazingira tuliyo wapata, yalikuwa nihatarishi sana.Bibi yangu alianza kuwafanyia matibabu hadi afya zao zikawa salama”
“huyo mtu wapili alikuwa ni nani?”
“ni sheila, ambaye kwa sasa, anaishi kwa mama”
“ahaa sasa ilikuwaje kwa mzee godwin”
“sasa hapo ndipo nilipopata kujua kwamba, mchongo wote wakutekwa kwa mama yako, aliyesababisha kutekwa kwake ni mzee godwin ambaye kwa sasa, ananyea debe gerezani”
Habari aliyo nipa john, ikajenga furaha iliyojawa nashauku yakutaka kutaka kumuona mama yangu,
 
“kwenye ndege umesha ajiriwa au bado?”
“ndio ninamalizia mafunzo,”
“kwa nini umekuwa muuhudumu wa ndege wakati, mipango yetu ilikuwa ni kuwa madaktari bingwa?”
“kaka, pcb mbaya mwanangu, nilizungusha”
“ulizungusha…..!!?”
“ndio ndugu yangu, nilipata zero, ila sijutii sana kwani muda mwingi niliutumia sana na catherina”
“na huyo catherina alipata ngapi?”
“ahaaa naye  pia alizungusha, japo alikuwa hkl, ila alizungusha”
“poleni sana”
“asate, eheee na wewe umemtolea wapi huyu bibie muarabu si muarabu, mzungu si mzungu?”
 
Nikaanza, kumuadisia john mkasa mzima wa maisha niliyo pitia kuanzia siku nilipokuwa nikitafutwa tanzania na kukimbilia nchini kenya ambapo ndipo, safari yangu yakwenda nchini iraq ilipo anza, nikamuelezea jinsi nilivyokutana na phidaya, na alivyokuwa msaada mkubwa sana kwenye masha yangu
“ninampenda sana phidaya”
“unauhakika?”
“ndio, asilimia mia”
“mmmmm  ni yule eddy ninaye mjua mimi, au kwa maana wewe ulikuwa mzee wa gologolo”
“hahaaaa, nimkekuwa mtu wangu, hapa nipo kwenye majukumu yakuitwa baba”
“safi ndugu yangu, ila nakutobolea siri moja?”
“siri gani?”
“sheila anakupenda sana, na hapa yupo anakusubiria wewe”
“mmmmm,”
 
Nilijikuta nikiguna, huku mapigo yamoyo yakianza kunienda mbio, mwili mzima ukaanza kusisimka, na nywele kichwani zikaanza, kunisisimka, jambo ambalo kwenye maisha yangu halikuwahi kutokea siku hata moja.Nikasimama haraka huku akilini mwangu nikmfikiria phidaya
“eddy unakwenda wapi?”
“chumbani”
 
Nilizungumza huku nikizidi kupiga hatua za haraka, nikaingia kwenye lifti pamoja na john, ambaye alikuwa akinifwata kwa nyuma, ikasimama kwenye ghorofa ya tatu, kama jinsi nilivyo minya batani ya ghorofa hii ambayo niyatatu, nikaanza kukimbia kuelekea chumbani kwangu, nilipo muacha mke wangu akiwa amelala, wasiwasi mwingi ukiwa umenitawala, nikafika kwenye mlango wachumba changu, nikaufungua kwa nguvu, kitu cha kwanza kutazama nikitandani, nikastuka kukuta mke wangu hayupo huku shuka jeupe lililo tandikwa juu yakitanda likiwa limejaa damu nyingi, jambo lilizozidi kustua mimi na john            
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!