Saturday, October 1, 2016

Salome ya Diamond yafikisha views milioni 3 ndani ya wiki 1 YouTube

Video ya wimbo ‘Salome’ ya Diamond Platnumz na Raymond imefikisha views milioni tatu katika mtandao wa YouTube kwa kipindi cha wiki moja.
 
Salome imezidi kupata heshima kubwa ndani na nje ya nchi na inawezekana ikawa ni tofauti na mwenyewe alivyotegemea muimbaji huyo kufikisha idadi hiyo ya watazamaji kwa kipindi kifupi.
Kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameandika:

3 Million Views Now!!!!! Kwa mapenzi mnayo ionyesha Nyimbo hii Kwakweli sina cha kuwalipa zaidi ya kuwashukuru na kuwaombea kwa Mwenyez Mungu awafungulie kila jema mliombalo… Nawashkuru sana …..
Hii ni hatua nzuri kwa muziki wa Tanzania, kwani inaonyesha ni jinsi gani watanzania wameamka kusupport muziki wenye vionjo vya nyumbani.
 
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!