Thursday, October 13, 2016

Video: Tale atoboa siri ya usambazaji wa nyimbo za WCB, hawaanzi na redio, blogs wala runinga


 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba wiki hii alitembelea ofisi za WCB na kuonyeshwa mambo mbalimbali ambayo yanafanyika katika kila kitengo.
 
Moja kati ya sehemu ambayo muheshimiwa alipekekwa ni sehemu ambayo huwa mikutano kuhusu usambazaji wa kazi za wasanii wa WCB hufanyika.

Akiongea katika utambulisho huo, Babu Tale alisema wao katika usambazaji wa kazi za wasanii wao huanza kwa watu wa chini ambao wanapatikana mtaani.

“Hii ni ofisi ya watu wa creative,” alisema Tale katika ubambulisho huo. “Wakati wa kunatoa nyimbo mpya lazima tunakaa na kuwaza tunafanya nini na tutatoa kwa style gani ili tuanze kuukamata mtaa tunafanyaje kuhusu mtaa. Kwa hiyo tunapotoa nyimbo tunahakikisha kila mtu mtaani anayo halafu ndio tunaiachia redioni. Kwahiyo ikienda redioni watu wa mtaa watakuwa wanaisukuma ile ya redio,”

Pia Diamond alisema wanaitegemea mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa katika kusambaza nyimbo zake kwa uharaka zaidi.

Kwa upande wa Waziri January Makamba alimmwagia sifa Diamond pamoja na team yake kwa kufanya kazi nzuri.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!