Thursday, October 13, 2016

Zitto Kabwe ampiga dongo Makonda kuhusu uchafu uliokithiri Coco Beach

Zitto Kabwe ameitupia lawama manispaa ya Kinondoni pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kushindwa kudhibiti tatizo la uchafu katika fukwe za Coco Beach.

Amedai kuwa ni aibu kuwa manispaa hiyo inayoongozwa na chama cha upinzani ndani ya mkoa unaoongozwa na kijana, kushindwa kuhakikisha usafi katika fukwe hizo maarufu. 
 
“Uchafu wa namna hii kwenye Manispaa inayoongozwa na Chama cha Upinzani ni aibu,” Zitto ameandika kwenye picha za fukwe hizo alizoweka kwenye mtandao wa Facebook.

“Lakini ni aibu zaidi uchafu wa namna hii kuwa katika mkoa unaoongozwa Na Mkuu wa Mkoa kijana katika mahala anapopita Kila Siku kwenda nyumbani kwake Na kwenda kazini,” ameongeza.
 
“Hapa Ni Coco Beach kwenye Mihogo. Hata sheria ndogo tu ya Manispaa ya kuwataka wenye shughuli hapa kusafisha mbele ya eneo Lao ingeweka mahala hapa kuwa safi. Kuna mambo hayahitaji misaada ya wazungu wala Wafanyabiashara. Ni akili za kimaendeleo tu.”

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!