Tuesday, November 8, 2016

Jinsi wezi walivyoiba mtambo wa ATM wa Benki ya Equity

Polisi nchini Kenya katika mji mkuu Nairobi wamemkamata mlinzi wa Benki ya Equity na kumhusisha na wizi ulifanyika katika mtambo wa kutoa pesa, ATM. mwishoni mwa juma lilipita na kisha kutoweka. Wezi hao walitoweka na kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kwa sasa.

Wezi hao walichimba ukuta wa nyuma wa Benki hiyo na kutoweka na sanduku la uhifadhi wa fedha pamoja na mtambo mzima wa ATM, huku likiwa na fedha ndani yake.

Inasemekana wezi hao waliweza kuzima kamera za CCTV na pia kengele ya usalama kabla ya kutekeleza wizi huo.

Kamanda wa jimbo la Nairobi Japheth Koome amesema kwamba polisi walikuta mitungi ya gesi na vifaa vingine ambavyo hutumuka kukata chuma.

Kamanda alisema inashangaza kuona kwamba wezi wa siku hizi wanapata maarifa mapya na kufanya matukio utadhani kwenye filamu na kutadhalisha wizi wa mabenki umeendelea kubadilika kila siku.

Mwaka uliopita kwenye tukio lingine kama hilo, wezi walijifanya kama wakaguzi wa hesabu katika benki hiyo walitoweka na dola za Marekani 300,000.

 – BBC/Swahili
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!